Mhe Makalla akikagua eneo la Coco beach mara alipozuru katika fukwe hiyo.
- Amesema hatuwezi kuwa na fukwe ukikaa unaziba pua, fukwe ziwe safi zivutie
- Aagiza kuwaorodhesha wafanyabiashara wote waliojenga vibanda eneo la Coco mara moja na zoezi liishe leo
- Awaalika Wadau kama NMB, PEPSI, TBL, COCA na wengine wengi kumsaidia kutimiza dhamira yake
- Amuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuleta umeme wa uhakika katika eneo la Coco beach mara moja
- Atangaza neema kwa wafanyabishara wadogowadogo katika eneo hilo awataka kujiunga katika vikundi ili watumie fursa za mikopo ya 10%
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Agosti 24, 2021 amezuru eneo la Coco beach Kinondoni, Dar es Salaam.
Akiwa katika eneo hilo pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kinondoni, Ilala na Kigamboni alipata wasaa wa kulizungukia eneo hilo na kuongea na wafanyabiashara wenye vibanda mahali hapo.
Mhe Makalla amebainisha dhamira yake ya kuboresha fukwe zote za Dar es Salaam na maeneo ya wazi, kwa kuweka mazingira katika hali ya usafi wakati wote, ziwe ni beach zinazovutia utalii na sehemu nzuri za mapumziko.
Kwa hatua za awali Mhe Makalla ameagiza mara moja kuanza kwa zoezi la kuwaorodhesha wafanyabiashara wa eneo hilo na zoezi liishe leo Agosti 24, 2021 pia amewataka kuondoa hofu hakuna atakayenyang'anywa eneo bali kinachofanyika ni maboresho ili eneo hilo liwe kivutio cha Utalii na watu kupumzika.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema anawaalika wadau kama NMB, PEPSI, TBL, COCA na wengine kuunga mkono juhudi za Serikali na dhamira yake ya kuziendeleza fukwe hizo kwa maslahi Mapana ya Mkoa na Taifa.
Sambamba na hilo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Godwin Gondwe kuleta umeme Coco beach na kujenga ofisi ambayo watumishi wachache watutumia wakati wakiwa wanasimamia fukwe hiyo.
Mkuu wa Mkoa Pia ametangaza neema kwa wafanyabishara wadogowadogo wa eneo hilo kwa kuwataka kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na mikopo ya 10% inayotolewa katika Manispaa, amesisitiza kuanzia sasa vibaka hawana nafasi amuagiza kamanda wa Polisi Kinondoni kusimamia hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa