Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Oktoba 19, 2021 ameupongeza uongozi wa Machinga Mkoa wa DSM kwa kuendelea na zoezi la kuwapanga vizuri wamachinga Mtaa wa Msimbazi Kariakoo kwa kuwaondoa wafanyabiashara walioziba njia za watembea kwa miguu ikiwa ni kuunga mkono Serikali katika zoezi la Kuwapanga vizuri wamachinga.
Mhe Makalla ametoa hongera sana kwa Viongozi hao na hii unaonyesha kujitambua, na amewaomba kutorudi nyuma pamoja na Changamoto ndogo iliyojitokeza leo kwa vijana wachache walioleta fujo.
Mhe Mkuu wa Mkoa amewashukuru Jeshi la polisi kwa uharaka wao kuwahi eneo la tukio ili kuwalinda viongozi wa wamachinga.
Mhe Makalla amesema Dar es Salaam iliyopangwa vizuri inawezekana ameuomba uongozi wa Machinga kuendeleza ushirikiano na Serikali pamoja na kutoa Elimu katika siku 11 zilizobaki ili kila mfanya biashara afanye biashara sehemu sahihi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa