Tarehe 12/05/2017 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda alifanya ziara ya kukagua ujenzi wa wodi za kisasa za wazazi na watoto zinazoendelea kujengwa katika Wilaya tatu za Ilala – Amana Hospitali, Temeke – Temeke Hospitali na Kinondoni – Mwananyamala Hospitali.
Ujenzi huo wa majengo ya ghorofa tatu kwa kila jengo la wodi ya wazazi na watoto katika Wilaya hizo utawawezesha zaidi wakina mama 1350 na watoto wao kupata huduma za malazi wakati wa matibabu.
Wodi hizi zikikamilika zitasaidia kuondoa kero ya mlundikano kwa kina mama wajawazito na watoto wao katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Ujenzi huu ni kwa ufadhili wa wadau wa maendeleo ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa