Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge leo tarehe 24 Agosti, 2020 ametembelea miradi ya DAWASA iliyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam ili kuweza kuona utekelezaji wa miradi hiyo yenye lengo la kumtua mama ndoo kichwani.
Awali, Mhe. Mkuu wa Mkoa akiambatana na Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja walianzia katika mradi wa Ujenzi wa Tanki la lita million 15 linalopokea maji kutoka katika visima vya Kimbiji na Mpera lililopo kisarawe 11 lenye thamani ya Shilingi Billioni 30 ambapo litasambaza maji kwenye maeneo ya Wilaya ya Kigamboni.
Baada ya hapo msafara wa Mhe. Mkuu wa Mkoa ulielekea katika mradi wa maji kutoka Kisarawe kuja Pugu Station unaogharimu kiasi cha Shilingi Billion 6.9 ambao utakuwa na uwezo wa kusambaza Lita million 5 kwa Zaidi ya wananchi laki nne wa maeneo ya Chanika, Majohe, Buyuni, Gongo la Mboto, Kigogo na Pugu.
Mhe. Mkuu wa Mkoa pia ametembelea mradi wa Mabwepande mpaka Changanyikeni unaogharimu kiasi cha Shilingi Billioni 67 unaokwenda sambamba na ulazaji wa mabomba ya maji kwa urefu wa km 1700. Huu mradi umefadhiriwa na Benki ya Dunia.
Baada ya kujionea na kupata maelekezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa DAWAS na Wakandarasi wa miradi hiyo Mhe. Kunenge alipata nafasi ya kuongea ambapo aliwapongeza DAWASA kwa utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwataka kukamilisha miradi yote kwa wakati. Aidha, aliwataka kuwafahamisha wananchi kuhusu miradi iliyopo katika maeneo yao. Zaidi aliwataka kuhakikisha upotevu ma maji unazuilika. Vilevile alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi nao walipe bili zao inavyotakiwa na kwa wakati.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja aliwahakikishia wananchi wa Dar es Salaam kuwa shida ya maji sasa inakwenda kuisha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa