MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MHE. PAUL MAKONDA APOKEA MWENGE WA UHURU.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi mara baada ya kumaliza shughuli za uzinduzi na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Lindi.
Mwenge huu wa Uhuru utakuwepo Mkoani Dar es Salaam kwa siku tano kuanzia leo tarehe 27/05/2017 hadi tarehe 31/05/2017 ambapo pamoja na mambo mengine zaidi ya miradi ipatayo arobaini (40) ya kimaendeleo yenye thamani ya Tshs 244,392,530,334/= itapitiwa, ambapo miradi mikubwa kumi na mbili (12) itazinduliwa, vilevile miradi mitano (5) itawekewa mawe ya msingi, pia miradi miwili (2) itafunguliwa rasmi na miradi kumi na moja (11) itatembelewa katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.
Katika hotuba yake kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Makonda amewahamasisha wananchi wake kudumisha Umoja na Mshikamano, Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria na Maambukizi ya VVU/UKIMWI na kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya Madawa ya kulevya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa