Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge ameendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Jiji la Dar es Salaam ambapo leo ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Daraja uliopo Ilala na ujenzi wa Barabara iliyopo katika Wilaya ya Temeke.
Awali RC Kunenge akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng’wilabuzu Ndwata Ludigija walitembelea katika Daraja la Kivule linalojengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya Nyanza ambapo amemtaka mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ifikapo Septemba 30 ili kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa eneo hilo.
Ameeleza kuwa kukamilika kwa Daraja na Barabara hiyo ni muhimu sana kwani barabara hiyo inakwenda mpaka katika Hospitali ya Wilaya ya Ilala.
Baada ya kutoka katika Wilaya ya Ilala msafara wa Mhe. Mkuu wa Mkoa ulielekea katika Wilaya ya Temeke ambapo ulielekea katika Barabara ya Mbosi kujionea ujenzi wa barabara hiyo unavyoendelea.
Baada ya ukaguzi wa barabara hiyo na kupokea taarifa kutoka kwa Mkandarasi wa barabara hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa aliagiza barabara hiyo kukamilika ndani ya mwezi mmoja na kumtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kutoa fedha za kumalizia ujenzi wa barabara hiyo ili ikamilike kwa wakati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa