Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amezindua Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI kwa mwaka 2016.
Akizindua Mkutano huo wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI kwa mwaka 2016 DC Mjema ameeleza kuwa utafiti huo unatija kubwa kwa jamii na unahitaji uhamasishaji mkubwa kwa wataalamu ili wananchi wakubali kupimwa kwa hiari yao wenyewe bila kulazimishwa na upimaji huo uzingatie usiri baina ya wataalamu na wananchi watakaopimwa.
Akizungumzia utafiti huo DC Mjema ameeleza kuwa utafiti huo ni wanne kufanyika hapa nchini uliolenga kuangazia masuala ya afya na utafiti, utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003/2004 na wapili ulifanyika mwaka 2007/2008 na watatu ulifanyika mwaka 2011/2012, na tafiti hizo zimekuwa zikihusisha wananchi wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49, na kuhusu tafiti za mwaka huu 2016/2017 DC Mjema ameeleza kuwa utakuwa wa kipekee kwani utahusisha wananchi wa rika zote katika kaya zilizochaguliwa.
Huku akifafanua kuwa ni utafiti wa kwanza kukusanya taarifa zinazohusiana na maambukizi mapya ya VVU, kiwango cha VVU mwilini kwa watu wanaoishi na VVU na wastani wa maambukizi ya VVU kwa watu wa rika zote na wingi wa chembechembe za kinga mwilini (CD4 T-cell count), uwepo wa viashiria vya usugu wa dawa, kiwango cha maambukizi ya kaswende na homa ya ini (Hepatitis B na C) kwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea, pia majibu ya vipimo yatatolewa papo kwa hapo.
Akizungumzia kiwango cha maambukizi ya VVU katika tafiti zilizopita DC Mjema ameeleza kuwa maambukizi yamepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003 mpaka asilimia 5.1 mwaka 2011, na kupelekea serikali kupunguza aslimia maambukizi ya VVU kwa aslimia mbili na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha chini cha maambukizi ya nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo nchi nyingi za ukanda huo zina kiwango cha zaidi ya aslimia 10.
Katika hatua nyingine DC Mjema amewaomba wataalamu kwa kushirikiana na vyombo vya habari kuendelea kuhamasisha ili wananchi katika kaya mbalimbali waweze kupimwa na kupata majibu papo kwa hapo kwani takwimu za majibu hayo zinaisadia serikali kutunga sera na kuandaa mikakati mipya ya kudhibiti UKIMWI, kuimarisha mpango wa ufuatiliaji na tathmini kwa miradi mbalimbali ya UKIMWI, kuboresha juhudi kubwa zinazofanywa na serikali za kusogeza huduma zinazohusiana na VVU, na hatimaye kujua ukubwa wa tatizo la UKIMWI na kuimarisha huduma.
Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI kwa mwaka 2016 umeudhuliwa na wawakilishi kutoka TACAIDS, Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS, ICAP, CDC na Makatibu Tawala wa Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa