Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Abubakar Kunenge amesema Mkoa huo umeendelea kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha unaendelea kuongoza kitaifa katika suala zima la ukusanyaji wa mapato pasipo kuwabugudhi wananchi kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato.
Akizungumza wakati wa kikao cha kutoa maoni ya mikakati ya kuboresha mapato ya Serikali katika mkoa wa Dar Es Salaam ulioshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Watafiti, Wataalamu na Taasisi mbalimbali, Bw. Kunenge amesema mkoa huo una kila sababu ya kuwa kinara wa ukusanyaji mapato hivyo Serikali ya mkoa itahakikisha wanaendelea kuwa kinara.
Aidha Bw.Kunenge amesema ndani ya Mkoa huo wapo wataalamu, watafiti, vyuo na makampuni ya ushauri ambayo mawazo yao yakitumika vizuri yataweza kusaidia kuongoza mapato.
"Tumeona tunaweza kufanya vizuri hivyo tumetumia nafasi hii kuomba makampuni, watalamu, walimu wafanya biashara na wadau mabalimbali watakao tusaidia kutushauri katika suala zima la ukusanyaji wa mapato na kutoa maoni yao kutusaidia jinsi ya tuboresha kupata mapato ya Mkoa wa Dar Es Salaam ilikumsaidia Mh Rais Katika kukamiliaha miradi ya maendeleo" alisema Bw.Kunenge
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Joseph Simbakaria alisema anatoa pongezi kwa wafanya kazi wa Mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mhe.Paul Makonda kwa kufanya kazi nzuri ya ukusanyaji wa Mapato, na kuona umuhimu wa kukaa na wadau wa biashara kuangalia jinsi gani wanaweza kusaidia mapato ya Mji Mkuu wa Biashara Dar es Salaam.
"Napenda kutoa pongezi kwa wafanya kazi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mhe. Paul Makonda kwa kufanya kazi nzuri ya ukusanyaji wa Mapato, na kuona umuhimu wa kukaa na wadau wa biashara kuangalia jinsi gani wanaweza kusaidia kuongeza mapato ya Mji Mkuu wa Biashara japo Mji Mkuu ni Dodoma ila kibiashara ni Dar es salaam.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa