Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau wa kudhibiti taka hatarishi wa TINDWA MEDICAL AND HEALTH SERVICES leo wametoa mafunzo kwa Maafisa Afya na Maafisa Mazingira wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu uzingatiaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na agizo la Waziri wa Mazingira la usimamiaji wa udhibiti wa taka ngumu na hatarishi kwa wadau wanaokusanya taka hizo kwa ajili ya kutunza, kuzisafirisha, kuzirejeleza na kuzingatia taratibu kama zilivyoagizwa kwenye sheria ya mazingira na kanunini zake za mwaka 2009.
Mafunzo hayo yalihudhuliwa pia na wadau kutoka TFDA, TBS, OFISI YA MKEMIA MKUU na NEMC ambao walipata nafasi ya kuchangia mada mbalimbali juu ya udhibiti wa taka hatarishi katika Mkoa wa Dar es Salaam. Hata hivyo baada ya kupata mafunzo kutoka kwa Afisa Mazingira mshauri wa Mkoa Bw. Churchill Mjuni na Afisa Afya Mkoa Bw. Dennis Kamzolah kamati ilipata nafasi ya kutembelea eneo maalum lenye mitambo ya kisasa kwa ajili ya udhibiti wa taka hatarishi lililopo Kisarawe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa