- RAS Hassan Rugwa asaini Mkataba huo na Kampuni iliyoshinda zabuni "Estim Construction Co Ltd"
- Asema Mkataba ni wa miezi 18 awataka kufanya kazi Usiku na mchana
- Asisitiza Kiu ya Rais Samia ni Kuona Ujenzi unakamilika kwa wakati na wafanyabiashara wanatumia Soko hilo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg Hassan Rugwa leo Disemba 22, 2021 amesaini Mkataba wa Ukarabati na Ujenzi wa Soko la Kariakoo na Kampuni ya "Estim Construction Co Ltd" ambapo Mkataba huo umesainiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM.
Akiongea kabla ya kusaini Mkataba huo RAS Rugwa amesema ikubumbukwe kuwa Ukarabati na Ujenzi wa Soko hilo umetokana na Janga la moto ambalo liliunguza Soko hilo hivyo zikaundwa kamati na zikakamilisha ripoti yake zikaja na mapendekezo ya kukarabati Soko la awali na kujenga Jipya ili kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara.
Aidha kwa Upendo Mkubwa wa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ametafuta pesa za kuwezesha kujenga Soko hilo, na Mkoa umefuata taratibu zote za kizabuni ambapo leo tukio la kusaini Mkataba limefanyika, na Kiu ya Rais ni kuona kazi inafanyika kwa wakati na ubora ili wafanyabiashara waingie katika Soko hilo akifafanua RAS Rugwa
"Ningependa Watanzania wajue Soko la Kariakoo kwa historia lilisanifiwa na Wazawa kwa hiyo limebeba historia kubwa ya Kariakoo na Tanzania ndio maana halijabomolewa bali linakarabatiwa" Alisema RAS Rugwa
Kwa upande wa Mhandisi Darpan Pindolia ambaye ndiye Mkandarasi wa Kampuni ya Estim Construction Co Ltd amesema wanao uwezo mkubwa hivyo kazi itafanyika kwa kufuata makubaliano ya Mkataba
Tukio la kusaini Mkataba huo limehudhuliwa na Wakuu wa Idara, Wawakilishi kutoka Shirika la Masoko Kariakoo, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais na Watumishi Ofisi ya RAS
RAI IMETOLEWA KWA WANYABIASHARA KARIAKOO KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KIPINDI CHOTE CHA UKARABATI NA UJENZI WA SOKO LA KARIAKOO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa