-Asema vikao vya ulinzi wa mama na mtoto vitaketi mara nne kwa mwaka
-Abainisha watoto wa kiume wako kwenye hatari zaidi kufanyiwa ukatili
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Toba Nguvila ametaka kuendeleza mapambano dhidi ya ukatili wakinamama na watoto katika Mkoa huo kwa kuwa mkoa una idadi kubwa ya watu na muingiliano mkubwa wa watu hivyo ni vema kwa umoja wetu kushirikiana kutokomeza janga la ukatili hususani kwa kinamama na watoto " lakini sio kweli kwamba wanaume hawafanyiwi ukatili bali mwanaume akifanyiwa ukatili hatoi taarifa hivyo ni vizuri kwenda mbali zaidi ili kuwasaidia wanaume pia" Alisema Dkt Toba
Katibu Tawala wa Mkoa ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha kisheria cha kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha Dkt Toba amesema tunapaswa kufanya kazi kwa weledi, ubunifu katika kushughulikia maswala ya ukatili, ikiwa ni pamoja na kamati kufanya ziara katika wilaya za Mkoa kutoa elimu vilevile kufanya midahalo, vipindi vya elimu kwa umma katika TV na Redio.
Pia ni muhimu Kamati zihakikishe elimu ya ukatili katika jamii inafika hadi ngazi za chini kabisa katika mitaa, sambamba na hilo Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba amesistiza ushirikiano katika kuratibu taarifa za ukatili hasa kwenye suala la Takwimu.
Kwa upande wa Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa bwana Nyamala Elisha amemuahakikishia Katibu Tawala wa Mkoa kusimamia kikamilifu maelekezo na maagizo yake ili kuleta ustawi katika jamii hususani wakazi wa Mkoa huo.
Mwisho baada ya kufunguliwa kikao hicho mada mbalimbali zimewasilishwa kwa lengo la kuijengea uwezo kamati hiyo ya ulinzi wa mwanamke na mtoto dhidi ya ukatili
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa