-RC Chalamila asema bila Amani ni vigumu kufanikisha malengo ya maendeleo.
Maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam wamejitokeza kwa wingi Leo Septemba 28, 2024 kuadhimisha siku ya Amani katika Viwanja vya Mwembe yanga jijini humo.
Akihutubia wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila amesema kila ifikapo tarehe 21 Septemba Dunia huadhimisha maadhimisho ya siku ya Amani duniani kutokana na uingiliano wa ratiba Mkoa unaadhimisha maadhimisho haya Leo Septemba 28,2024.Siku hii ni muhimu kwakuwa ina kumbusha watu kuhusu umuhimu wa kutatua migogoro kwa njia za amani,kuzuia vita, kuimarisha mshikamano na umoja miongoni mwa jamii.
Vilevile ni fursa adhimu ya kuangazia maswala ya haki, usalama na maendeleo endelevu ili kujenga Taifa bora kwa Kila mtu .
Aidha RC Chalamila amesema ni muhimu kulinda na kudumisha Amani tuliyonayo,bila Amani ni vigumu kufanikisha malengo ya maendeleo.
Sambamba na hilo RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta 4R ikiwemo maridhiano kama nguzo ya amani katika Nchi yetu pia, ameelezea lengo la maadhimisho hayo ni kutoa fursa ya kuhamasisha watu kujenga uelewa juu ya maswala ya amani, umoja na ushirikiano.
Katika maadhimisho hayo viongozi wa dini walipata wasaa wa kuzungumza na kutoa nasaha kwa wananchi hasa kwenye maswala ya kudumisha Amani kwenye Taifa letu ambapo Shekh Yahaya ambaye ni muwakilishi wa mashekhe wa Mkoa wa Dar es salaam ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kusimama kidete na kuonesha hekima na busara kuilinda nchi iendelee kuwa na Amani hususani Mkoa huu jambo ambalo limeungwa mkono na viongozi wengine toka madhehebu mengine.
Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Toba Nguvila wakati anamkarbsha mgeni rasmi Mhe. Albert Chalamila amesema nia ya maadhimisho hayo ni kuimarisha amani katika Mkoa huo na Taifa kwa ujumla na hata kusaidia kutatua migogoro katika jamii kwa kuwa wamoja hususani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi Novemba 27,2024.
Mwisho, Licha ya wananchi wengi kujitokeza katika maadhimisho hayo viongozi mbalimbali wamejitokeza pia, ikiwemo Wakuu wa Wilaya,wastahiki meya , Wakuu wa Taasisi, Makatibu Tawala wa Wilaya zote tano ,viongozi wa dini, wazee na watu mashuhuri na kupambwa na burudani kadha wa kadha kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili kama vile Bahati Bukuku na makundi maalumu yaliyosherehesha kwa kiwango kizuri
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa