Maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Ilala leo wamejitokeza kwa wingi kuitika wito wa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Makonda wa utatuzi wa migogoro ya ardhi ambapo wamepongeza kuona migogoro yao ambayo mingine ni sugu inapatiwa ufumbuzi na majibu ya papo kwa papo.
RC Makonda amesema mkoa huo umeamua kufunga mwaka kwa kusikiliza kero za migogoro ya ardhi na utoaji wa hati za makazi ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na uhakika wa makazi.
Aidha RC Makonda amesema shauku yake ni kuona maeneo yote ya jiji la Dar es salaam yanapimwa na wananchi kupatiwa hati za makazi ili kupunguza migogoro ya viwanja, mashamba, mipaka, fidia na utapeli wa watu kuuziwa eneo moja zaidi ya watu wawili jambo linaloleta usumbufu kwa wananchi.
Ziara hiyo ya siku tano za utatuzi wa migogoro imeanza rasmi leo chini ya usimamizi thabiti wa Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi na RC. Makonda inalenga kupunguza migogoro ya ardhi
iliyowasumbua wananchi kwa muda mrefu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa