Katibu Tawala Mkoa Bi Rehema Madenge Akionyesha Batiki ambayo itakuwa Vazi rasmi katika maadhimisho hayo.
-RAS Madenge amesema maadhimisho hayo yameanza leo Machi 6, 2023 katika viwanja hivyo na kilele chake ni Machi 8,2023
- Ataja Vazi rasmi litakalovaliwa katika maadhimisho hayo ni Batiki
- Akaribisha wanawake wote DSM na wadau kushiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Katika Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi Rehema Madenge amesema maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Mkoa wa Dar es Salaam mwaka huu yakichagizwa na kauli Mbiu " Ubunifu na mabadiliko ya Kiteknolojia, Chachu katika Kuleta Usawa wa Kijinsia " yatafanyika katika viwanja wa Mnazimmoja Ilala Jijini Dar es Salaam
Ameyasema hayo leo Machi 6, 2023 wakati akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake Ilala Boma.
Katibu Tawala wa Mkoa huo amesema maadhimisho hayo yameanza leo Machi 6, 2023 hadi Machi 8, 2023 yakipambwa na maonesho ya bidhaa mbalimbali za kijasiriamali ambazo zinatengenezwa na wanawake .
Aidha amesema katika maadhimisho hayo mwaka huu vazi rasmi litakuwa ni Batiki ambayo imetengenezwa na Wanawake wajasiriamali wa kitanzania, lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi zao katika kujiletea maendeleo
Sambamba na hilo Katibu Tawala wa Mkoa ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wanawake na Wananchi wote wa DSM kwa Ujumla kushiriki katika maadhimisho hayo katika viwanja vya Mnazimoja ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla
Ifahamike kuwa siku ya Kitaifa ya Wanawake Duniani ilianza mwaka 1911kufuatia maandamano ya Wanawake wafanyakazi wa viwandani nchini Marekani waliokuwa wakipinga mazingira duni ya Kazi kama vile ukosefu wa huduma za kijamii na unyanyasaji katika ajira, hivyo kuendelea kuadhimisha Siku hiyo ni kuenzi mchango wa Wanawake katika Ujenzi wa Taifa husika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa