-Tamasha kubwa kufanyika April, 25, 2024 katika viwanja vya Tanganyika Peckers Kinondoni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo April, 24, 2024 akizungumza na vyombo vya habari Ofisini kwake amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafikisha miaka 60 ifikapo ijumaa April 26 mwaka huu, sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanzania kitaifa zinafanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Katika sherehe za maadhimisho hayo mgeni rasmi ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na Viongozi mashuhuri kutoka nchi mbalimbali wamealikwa kuhudhuria sherehe hizo muhimu kwa Taifa letu.
Aidha RC Chalamila amesema maadhimisho hayo yatapambwa na Shughuli mbalimbali ikiwemo gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama pamoja na burudani kutoka kwa wasanii maarufu hapa nchini.
Vilevile tarehe 25, April 2024 katika viwanja vya Tanganyika Peckers Wilaya ya Kinondoni kutakuwa na Tamasha kubwa la kihistoria kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Doto Biteko katika Tamasha hilo kutakuwa na burudani kabambe kutoka kwa wasanii wakubwa nchini akiwemo Zuchu, Diamond, Alikiba, Hamonize na wengine wengi.
Pia Mhe Mkuu wa Mkoa amesema April 25, 2024 kuanzia saa 11 jioni kutakuwa na burudani hadi itakapofika saa 3 usiku washiriki watapata fursa ya kusikiliza Hotuba ya Kihistoria mubashara kupitia Television, hivyo washiriki watafuatilia hotuba hiyo katika Luninga kubwa zitakazowekwa uwanja wa Tanganyika Peckers.
Mwisho RC Chalamila amewataka viongozi na Wananchi wa Mkoa huo kuhudhuria kwa wingi kuanzia kesho siku ya Tamasha na April 26, 2024 katika uwanja wa Uhuru kuanzia saa 12 asubuhi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa