Kuelekea siku ya Maadhimisho ya magonjwa yasiyoambukiza Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana na vikundi Mbalimbali vya jogging katika Manispaa hiyo, imefanya mazoezi ya kukimbia (jogging) lengo ikiwa ni kuhamasisha jamii kufanya mazoezi kama njia bora ya kuepuka magonjwa hayo.
Mazoezi hayo yaliyoongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo yalianzia Hospitali ya Wilaya iliyopo Kimara Baruti hadi Daraja la Kijazi ( kijazi Interchange)
Akiongea baada ya mazoezi hayo Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bwana aliwaeleza wananchi kuwa mazoezi ni afya hivyo kila mtu anapaswa kufanya ili kuimarisha afya zao na hivyo kuepuka magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo
Aidha, Mkumbo alisema mazoezi hayo pia yamelenga kuwaeleza wananchi juu ya ufunguzi wa Hospitali ya Wilaya hivi karibu ambapo wananchi wameshiriki kupanda miti na kuchangia damu ikiwa maandalizi ya ufunguzi wa Hospitali hiyo.
Pia wananchi wamehamasishwa kuchanja kwa hiari chanjo ya UVIKO -19 kwa ajili ya kujinga na ugonjwa huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa