Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama ameyasema hayo leo Novemba 22, 2023 akiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila walipotembelea maeneo ya Mwanagati kata ya Mzinga kuona athari za mvua zinazoendelea.
Mhe. Mhagama amewata Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) waanze ujenzi wa kukarabati kivuko hicho mara moja ili wananchi waendelwe kupata huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi za kila siku ziendelee hivyo wahakikishe miundo mbinu ipo salama.
"Milioni 20 haraka ziende kwenye kivuko chetu hapa Mwanagati zianze kazi haraka sana, tunataka kivuko hiki kipitike muda wote," alisema Waziri Mhagama huku akitoa angalizo pesa hivyo zitumike kama zilivyopangwa na wananchi washirikishwe.
Pia Waziri Mhagama alisema serikali haiwalazimishi wananchi wanaoishi mabondeni wahame ila kwa hiyari yao, "Lengo letu ni kila mmoja aanze kuchukua tahadhari yeye mwenyewe, wale wanaoishi kwenye nyumba ambazo zipo kwenye mkondo wa maji usisubiri nyumba yako mlango ufunguliwe na maji, fungua wewe mwenyewe, mvua haina undugu."
Vilevile mhe Mhagama waliwataka viongozi na wananchi wachukue tahadhari ya magonjwa ya milipuko yanayoweza kutokea kipindi hiki cha mvua ikiwemo kuharisha na malaria hivyo wazingatie usafi wa mazingira na washirikiane pamoja kusafisha na kutoa elimu kwa wasioelewa.
Naye Mhe. Chalamila alitoa pole kwa wakazi wa eneo hilo kwa athari za mvua zinazowakumba na alimweleza Mhe. Waziri kwamba wananchi wanachoomba ni miundo mbinu, "Kikubwa zaidi kinacholiliwa hapa likishatengenezwa daraja hatua inayofuata ni barabara."
Pia RC Chalamila alisema ujenzi msambao/holela bado ni changamoto na mji huo unakua kwa kasi sana hivyo huduma za miundo mbinu lazima serikari iwajengee na eneo hilo la Mwanagati linahitaji mkakati mpana kama Mhe. Waziri ulivyojionea mwenyewe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa