Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam RCC kimeguswa na kazi kubwa inayofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda katika kushughulikia kero za wananchi kupitia Sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, Ulinzi na usalama pamoja na sekta nyinginezo.
Akifungua kikao cha RCC Mkoa kwa niaba ya RC Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema amesema Mkoa wa Dar es salaam umepiga hatua kubwa kwenye Maboresho ya sekta ya Afya kupitia ujenzi wa majengo ya Hospital ikiwemo Wodi ya Mama na Mtoto Hospital ya Amana, Ujenzi wa Hospital ya Mama na Mtoto Chanika, Ujenzi wa Jengo la Upasuaji kwa Wajawazito Hospital ya Mwananyamala na jengo la wagonjwa wa dharura Hospital ya Temeke zote hizo zikiwa ni jitiada binafsi za RC Makonda.
Aidha Bi. Mjema amesema kwenye sekta ya Elimu Mkoa umeendelea kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa na sasa RC Makonda yupo kwenye kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu yote ikiwa ni kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu.
Aidha Mjema amesema licha ya kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano bado zipo changamoto mbalimbali zinazokabili mkoa ikiwemo Ujenzi holela, Biashara holela, Ombaomba, watoto wa mtaani na uchafuzi wa Mazingira ambapo tayari RC Makonda ameshaagiza kila Halmashauri itenge fedha za ununuzi wa mitambo ya usafishaji wa mazingira katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017-2018.
Hata hivyo Bi. Mjema amesema Mkoa umeweza kuwatambua watumiaji wa madawa ya kulevya zaidi ya 6,000 ambapo Kati ya hao 2,000 wamepatiwa ushauri jinsi ya kuacha dawa za kulevya na 1,700 wanatumia methadone, na wengine 250 wako sober house hizi zote zikiwa ni jitiada za RC Makonda kuokoa nguvu kazi ya vijana waliokuwa wakipotea kutokana na matumizi ya dawa za kulevye.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa