Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando amefanya kikao na Wachumi, Wakuu wa Vitengo vya TEHAMA na Maafisa Habari katika Mkoa wa Dar es Salam.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Ilala na kuhudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Makatibu Tawala wa Wilaya.
Akifungua mkutano huo Katibu Tawala wa Mkoa amesema kikao hichi ni muhimu ambapo kinawaunganisha wataalamu wa sekta hizo kuzungumzia namna ya kuboresha utendaji wa kazi za kila siku.
Amesema nimewaita kada tatu tofauti nikiamini kuwa kila mmoja anatekeleza majukumu yake lakini ipo haja ya kuwa na uhusiano wa ukaribu katika utendaji wa kazi zenu kwani Maafisa Habari wanapaswa kuandika habari za ukweli na uhakika zinazotoka katika Idara ya Uchumi zinazoelezea uwepo wa shughuli za maendeleo ya kiuchumi na uwekezaji katika Mkoa wetu.
Aidha Katibu Tawala amewataka Maafisa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwani kuna mambo mengi yanafanywa katika mkoa wetu lakini hayafiki kwa wananchi. Amewataka kutumia REDIO YA JIJI inayoitwa CITY FM yenye masafa ya 91.7. Amesema “Tunayo Redio yetu ya Jiji ambayo tunapaswa kuitumia kikamilifu kwa kuelezea yaliyomo katika Mkoa wetu kwani tunazo shughuli nyingi zinafanyika lakini hazisikiki”. Tupange utaratibu mzuri na endelevu wa kwenda katika RADIO YA JIJI angalau siku moja moja kutoka katika Halmashauri zetu na Mkoa ili kuelezea yaliyomo katika sehemu/maeneo yetu.
Kwa upande wa Makatibu Tawala wa Wilaya nao pia washaurianae na Halmashauri za Manispaa zao mambo yafuatayo:-
Wachumi kuwapatia Maafisa Habari taarifa zinazotoka katika sehemu zao kwani kuna mambo mengi sana yapo na hawajayatoa bado kwa wananchi.
Aidha, ilishauriwa wajitahidi kukuza ushirikiano kati yao na Maafisa Habari kwani itawarahisishia kufikisha taarifa kwa wananchi kwa urahisi.
Kwa upande wa Maafisa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam walikubali na kuazimia kuwa kuanzia sasa na kuendelea watafanya mapinduzi makubwa ya kihabari kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.Waliahidi kutumia REDIO YA JIJI ipasavyo sambamba na kuanza sasa kuandaa Makala, Vipeperushi, Majarida na Documentary mbalimali.
Katibu Tawala wa Mkoa alimaliza kikao chake kwa kuwataka watumishi wote kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwani kila mmoja akitimiza wajibu tutapunguza kero ambazo wananchi wanailalamikia Serikali yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa