- Asema tarehe 4/12/2021 Kampeni ya Usafi wa pamoja DSM itazinduliwa Rasmi
- Afafanua Usafi wa pamoja kwa mwezi DSM Utafanyika mara moja kuanzia saa 12:00 hadi 3:00 Asubuhi
- Aeleza Jinsi ya kutekeleza zoezi hilo kutokana na swali aliloulizwa kuwa siku ya Jumamosi wengine huitumia kufanya mambo mengine ikiwemo Mazoezi hivyo itakuwaje?
- Asisitiza mambo manne (4) katika Utekelezaji wa Zoezi la Usafi DSM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Novemba 23, 2021 akiwa katika Kipindi cha 360 kinachorushwa na Runinga ya Clouds TV nyumbani kwake Masaki Kinondoni -Dar es Salaam.
Mhe Makalla ameeleza kampeni yake ya Usafi DSM ambapo siku ya jana Novemba 22 alizindua Mpango endelevu wa usafi katika Mkoa wa Dar es Salaam ukiwa na kauli mbiu ya SAFISHA, PENDEZESHA DAR ES SALAAM
Mkuu wa Mkoa ametangaza siku rasmi ya uzinduzi wa kampeni ya usafi ambayo ni tarehe 4 ambapo Usafi Utafanyika kwa pamoja, na hiyo itakuwa ni namna mojawapo ya kuadhimisha wiki ya Kuelekea sikukuu ya Uhuru wa Tanzania, 9 Disemba.
Aidha Mkuu Mkoa amesema ametangaza usafi kufanyika kwa mwezi mara moja haimaanishi kwamba Siku zingine watu wasifanye usafi " Usafi ni Kila Siku lakini Usafi wa pamoja ndio Utafanyika kila Jumamosi na hiyo inatoa fursa ya kuweza kujumuika pamoja na majirani.
Vilevile amejibu swali aliloulizwa kuwa watu wamekuwa na ratiba za kufanya mamboo mengine ikiwemo Mazoezi itakuwaje kwa tamko lake la kuwataka wakazi wa DSM kufanya usafi kuanzia Saa 12 00 hadi Saa 3: 00 Asubuhi kwa mwezi mara moja?
Mhe Makalla amejibu kwa kusema katika familia kuna watu zaidi ya mmoja hivyo haoni sababu ya jamii kushindwa kutekeleza zoezi hilo akitolea mfano tunao madaktari au manesi au wanaoenda mchinjio asubuhi, kikubwa sheria lazima ifuatwe. Mmoja hayupo uwakilishi wa familia utakuwepo na zoezi la usafi litafanyika.
Mhe Makalla amebainisha mambo mnne ambayo yanaenda sambamba katika Utekelezaji wa Zoezi la Usafi DSM kwanza Kudhibiti ufanyaji holela wa biashara pili Kusimamia vizuri matumizi ya Sheria za Mazingira, tatu Kasi ya Ukusanyaji na Uteketeshaji wa Taka kwa kuzingatia teknlojia ya kisasa na nne Uhamasishaji na Elimu kwa Jamii
DAR ES SALAAM NDIO USO WA NCHI, NDIO LANGO, NI WAKATI SAHIHI WA KWENDA NA KAULI MBIU YA "SAFISHA, PENDEZESHA DAR ES SALAAM
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa