Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Mhe Albert Chalamila* leo Oktoba 20,2023 ametoa taarifa ya kamati aliyounda kuchunguza tukio la Janga la moto lililotokea eneo la Mnadani Kariakoo mnamo Oktoba 1, 2023
RC Chalamila amesema kamati hiyo imefanya kazi ya Uchunguzi ndani ya siku saba (7) kuanzia Oktoba 07, 2023 na kubaini chanzo cha moto huo sio ajali bali ni HUJUMA ndani ya wafanyabishara wa Mnadani Kariakoo ambapo ameziagiza Mamlaka husika kuwabaini watu hao na kuwachukulia hatua Stahiki za kisheria.
Uchunguzi huo umehusisha ukaguzi wa eneo la tukio, kufanya mahojiano na mashuhuda, wamiliki wa majengo yanayozunguka eneo hilo, wafanyabishara,walinzi wa zamu na picha za kamera zilizorekodi tukio hilo kabla na baada ya tukio la moto huo
Aidha kamati imetoa mapendekezo na ushauri ikiwemo wafanyabishara kutafutiwa eneo mbadala la kuweza kuendesha Shughuli kutokana na aina ya biashara zao kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam,pia Halmashauri kusimamia sheria za mipango miji kwa mfano kuacha njia moja kati ya jengo moja na jingine pia waliokua wanaziba njia watambuliwe na kuchukuliwa hatua za kisheria, BRELA ifanye mapitio ya Kampuni ya The Kariakoo Auction Mart Co Ltd ili kupata uhalali wa umiliki na namna ya uendeshaji wa Kampuni hiyo.
Hata hivyo kufuatia janga hilo la moto kamati imebaini kusababisha madhara kadhaa ikiwemo kuungua na kuteketea kwa eneo lote la biashara la Mnadani vibanda vya biashara zaidi ya 550 pamoja na mali zikiwemo maduka/ fremu kumi (10) majengo marefu Saba( 7) yaliyozunguka eneo hilo kwa upande wa athari za kibinamu hakukuwa na kifo chochote, bali kulitokea majeruhi ya watu sita (6) kati yao watu wazima watano (5) na mtoto mmoja (1)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa