Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda anakualika kushiriki katika Sherehe ya Ufunguzi wa Flyover ya Mfugale itakayofanyika kesho tarehe 27/09/2018 saa mbili kamili asubuhi katika Makutano ya Barabara za Mandela na Nyerere eneo la Tazara ambapo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atakuwa mgeni Rasmi na Kufungua Daraja hilo.
Ikumbukwe kuwa Daraja hili la barabara ipitayo juu (Flyover) limejengwa chini ya ufadhili wa Serikali ya Watu wa Japan kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari. Ujenzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika Ibara 39 (g): Kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Licha ya kwamba flyover hii imejengwa Dar es Salaam,itakuwa ni kichocheo cha Maendeleo nchini kwani Jiji la Dar es Salaam ni jicho la Nchi na lango kuu la Uchumi. Hivyo wananchi tunapaswa kuitunza Miundombinu hii kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuifanya miradi mikubwa kama hii kuwa endelevu na hivyo kufanikiwa kufikia lengo la Taifa la kupunguza umaskini na kuweza kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ifikapo mwaka 2025.
TUMEAHIDI TUMETEKELEZA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa