IJUMAA KAREEM KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul C. Makonda leo amekutana na Masheikh na Viongozi wa Misikiti zaidi ya Mia Sita (600) ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Hatua hii ni muendelezo wa Mikutano yake na Makundi ya watu mbalimbali, katika kuuenzi Mwezi wa Mfungo wa Ramadhani.
Vilevile Mhe. Makonda ametoa vitu mbalimbali kama SADAKA KWA KILA KIONGOZI kwa kila Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ambavyo ni:-
Akizungumza na Masheikh na Viongozi wa Dini ya KIISLAMU, Mhe. Makonda ameanza kwa kuwapongeza kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali pamoja na kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa jinsi ambavyo anatekeleza utendaji wake wa kazi kwa kuhakikisha anaipeleka Tanzania kwenye nchi ya Uchumi wa kipato cha kati kupitia MAPINDUZI YA VIWANDA.
Mhe. Makonda pia amewaomba viongozi wa Dini kuutumia mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kuhubiri AMANI, UTULIVU NA KUVUMILIANA katika kila mambo wanayoyafanya waumini wao.
Katika hatua nyingine, Mhe. Makonda amefanikiwa KUWASHAWISHI wafanyabiashara haswa wa SUPERMARKET Mkoa wa Dar es Salaam kufanya kazi mpaka saa sita za usiku, ili kutoa fursa kwa wananchi kujipatia mahitaji yao muhimu kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa