Rais wa Shirika la Misaada la Korea Kusini KOICA Bi.Lee Mi Kyung amezindua Hospital ya Mama na Mtoto Chanika iliyojengwa kwa jitiada binafsi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda aliyetafuta wafadhili hao.
Ujenzi wa Hospital hiyo ya kisasa umegharimu zaidi ya Shillingi Billion 9.8 ambapo ndani kuna vyumba vya kisasa vya Upasuaji, vyumba vya Madaktari, Maabara,Chumba cha Mionzi, wodi ya wazazi,wodi ya watoto njiti, Theater, vyumba vya kujifungulia, ICU, Vyoo vya kisasa pamoja na nyumba za Familia 28 za madaktari ambapo ndani ya nyumba hizo kuna kila kitu.
RC Makonda amesema aliamua kutafuta wafadhili wa kujenga Hospital hiyo baada ya kuona kilio cha kinamama waliokuwa wakipoteza maisha na watoto baada ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya.
Aidha RC Makonda amemuomba Rais wa KOICA kumjengea Hospital nyingine mbili kwenye Wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni ili kusaidia maboresho ya huduma za afya.
Pamoja na hayo RC Makonda ameshukuru serikali ya Korea Kusini kwa ufadhili wa hospital hiyo yenye hadhi ya kimataifa.
kwa upande wake Rais wa KOICA Bi. Lee Mi Kyung amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo huku akipongeza Tanzania kwa kudumisha Amani tofauti na Mataifa mengine.
Uzinduzi wa Hospital hiyo umeenda sambamba na uzinduzi wa magari mawili ya kisasa ya wagonjwa (ambulance).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa