- Ni baada ya kufanya tathimini ya viashiria vya utoaji huduma BORA za Afya katika Mkoa.
- Tuzo zote mbili za utoaji huduma BORA wa Afya zanyakuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeongoza katika kufanya vizuri eneo la Afya kufuatia tathimini iliyofanyika ya kupima viashiria vya utoaji huduma BORA za Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam
Mkutano wa mwaka wa tathimini hiyo ya huduma za Afya umekuwa na lengo la kuona hali ya utoaji huduma za Afya na kuweka mikakati ya kuboresha zaidi huduma hizo katika hospitali za rufaa za Mkoa Mwananyamala, Temeke na Amana pamoja na vituo vya afya na Zahanati.
Kupitia tathimini iliyofanyika baadhi ya vigezo vilivyokuwa vinashindanishwa ni *Utoaji wa huduma bora ya mama na mtoto, Utawala na Fedha, utoaji wa dawa, Mahabara, Vifaa tiba, Mazingira bora, lishe na Ustawi wa Jamii
Tathimini hiyo katika nyanja ya CHMT ilionyesha Ilala Kushinda na kujipatia tuzo ya kwanza na ya pili ni upande wa Hospitali za Rufaa ambapo Amana imefanya Vizuri na kujinyakulia tuzo ya pili.
Akiongea wakati wa kukabidhi Tuzo hizo kwa washindi wa utoaji huduma BORA za Afya Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Ng'wilabuzu Ludigija* amepongeza utaratibu unaofanywa na Mkoa wa kuwa na tathimini ya mwaka na kupanga mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma BORA za Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mhe Ludigija amewataka wataalam wa Afya kuelewa kuwa ushindi walioupa Halmashauri ya Jiji hauna maana Wilaya zingine zinatoa huduma mbovu hiyo sio, bali yako maeneo Halmashauri ya Jiji inawazidi wengine, hivyo hiyo iwe fursa ya kuja kujifunza katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Aidha Amewataka kuboresha huduma za utoaji afya kwa wazee katika Hospitali na vituo vya afya DSM kwa kuwa kundi hilo linachangomoto kubwa ya uhitaji wa huduma bora za Afya.
Kwa Upande wa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Utumishi Bwana Lawrence Malangwa amewapongeza na kuwataka kuendelea na utaratibu wa kufanya tathimini ya utoaji huduma bora na kupanga mikakati ya kuboresha pale panapoonekana kulegalega kwa maslahi mapana ya Wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa