- Wananchi Wenye umri wa kuanzia miaka mitano na kuendelea wahimizwa kushiriki
- Wataalamu kupita nyumba kwa nyumba kutoa dawa.
Mkoa wa Dar es salaam unatarajia kuanza Kampeni ya ugawaji kingatiba ya kudhibiti ugunjwa wa matende/ mabusha (Ngirimaji) November 21-25 kwenye Wilaya za *Ilala, Temeke na Kinondoni ambazo zimeonekana kuathirika zaidi na tatizo Hilo.
Akizungumza wakati wa kikao Cha Wadau kuelekea Kampeni hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ludigija Ndatwa Ng'ilabuzu amesema lengo la Kampeni hiyo ni kuwafikia zaidi ya Wananchi milioni nne Wenye umri wa miaka mitano na kuendelea kwa jinsia zote.
Aidha Ludigija ametoa wito kwa Viongozi wa Mitaa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wataalamu wa Afya Watakaokuwa wakizunguka kutoa Kinga.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dr. Rashid Mfaume amesema chanzo Cha ugonjwa huo ni minyoo midogomidogo inayosababishwa na Mbu hivyo ni vyema Wananchi wakapata Kinga hiyo.
Aidha Dr. Mfaume amesema Kinga hiyo inatolewa *Bure na haina madhara yoyote kwa Wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa