Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa leo amezindua Kampeni ya kugawa Kinga Tiba za Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (Matende, Mabusha,Minyoo ya Tumbo na Ngiri Maji) kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Navy-Kigamboni .
Zoezi hili la kimkoa litaendelea mpaka tarehe 3/12/2017 ambapo wananchi wote wenye umri kuanzia Miaka mitano (5) na kuendelea wanapaswa kupata dawa hizi kwa ustawi mzuri wa afya zao.
DC Mgandilwa alishukuru uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuruhusu zoezi hilo kufanyika katika Wilaya yake na kuomba hatua hiyo isiishie hapo tu bali iwe endelevu.
“Afya zinapaswa kuwa njema kwa watanzania wote hivyo yatupasa kuunganisha nguvu zetu na kutumia rasilimali tulizonazo katika kupambana na magonjwa haya” Alisema DC Mgandilwa.
Aliongeza kuwa kwa kampeni hii ya leo tunakila sababu ya kujitoa kwa dhati kabisa kwenda kumeza dawa hizo kwani huduma hii mbali na kuwa ni muhimu kwetu lakini haina malipo yoyote na itatolewa katika Vituo vya mabasi, Masoko, Ofisi za Serikali, Ofisi za Kata, Wizara na Taasisi zote za Umma.
DC Mgandilwa amewaasa wananchi wote kujitokeza kumeza dawa. Aidha ameeleza kuwa katika utoaji wa huduma ya matibabu kituo cha Afya cha PUGU kinaendelea kutoa matibabu bure.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa