Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ludigija Ng'ilabuzu amelielekeza Jeshi la Zimamoto na uokoaji kuchukuwa hatua kwa Taasisi au Wananchi wanaokaidi maelekezo ya Jeshi Hilo hususani kuweka Vifaa vya kudhibiti moto kwenye maeneo ya Biashara na Majengo marefu.
DC Ludigija ametoa maelekezo hayo wakati wa kileleni Cha maadhimisho ya Zimamoto na uokoaji yaliyolenga kutoa Elimu kwa Wananchi ambapo maadhimisho hayo yamefanyika Viwanja vya Jeshi la Zimamoto Dar es salaam.
Aidha Ludigija amewataka Wananchi kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini tukio la moto ili kuwezesha Zimamoto kufika kwa wakati* na kuokoa Maisha ya Wananchi na Mali.
Hata hivyo ameelekeza DAWASA kushirikiana na Jeshi Hilo kujenga visima kwaajili ya kuhifadhi maji huku akiwataka TARURA nao kushirikiana na Jeshi Hilo kwa kuhakikisha Miundombinu ya Barabara zinapitika vizuri.
Pamoja na hayo amezielekeza *Halmashauri* kuweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha Masoko, Vituo vya Daladala, hospital na maeneo mbalimbali ya huduma za Jamii kunakuwepo na Miundombinu ya kuzuia moto
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa