Naibu Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso leo ameikabidhi DAWASA miradi miwili; ya majisafi na usafi wa mazingira.
Miradi hii iligharamiwa na Shirika la Water Aid Tanzania na kujengwa chini ya usimamizi wa Asasi ya PDF.
Akimwakilisha Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa katika hafla hio, Mhe. Aweso alikagua na kuzindua miradi hiyo muhimu kwa ajili ya wakazi wa Kibondemaji, Charambe na Toangoma Wilayani Temeke.
Mradi wa majitaka una uwezo wa kuchakata lita 50,000 Za majitaka kwa siku. Faida za mradi huo ni pamoja na upatiakanaji wa mbolea, maji kwa ajili ya Umwagiliaji na gesi ya kupikia.
Mradi wa majisafi una uwezo wa kuzalisha lita 224, za maji kwa siku na utahudumia wakazi wa Chharambe na Kibondemaji. DAWASA mkoa wa Temeke wameanza kuunganisha wananchi na huduma ya maji ya mradi huu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa