Mkoa wa Dar es salaam Leo August 20 umefanya Tamasha la Sensa Kama sehemu ya hamasa kwa Wananchi kujitokeza kushiriki zoezi Hilo linalotaraji kufanyika August 23 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa Tamasha Hilo lililofanyika Viwanja vya Posta Kijitonyama kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe ametoa wito kwa Wananchi kutoa taarifa sahihi kwa Makarani wa sensa.
Aidha DC Gondwe amesema Serikali tayari imekamilisha mahitaji yote muhimu ya kuratibu Zoezi Hilo ikiwemo Vifaa na Watumishi hivyo kilichosalia ni Wananchi tu kutoa ushirikiano.
Kwa upande wake Mratibu wa Sansa Mkoa wa Dar es salaam Albert Kapala amesema siku ya kesho August 21 Makarani wa sensa wataanza kuzunguka maeneo yao ya kazi kwaajili dodoso na utaambuzi wa mipaka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa