Mafunzo hayo ya siku 2 yamefunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Mipango na Uratibu Bwana Mozes Chillah kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Toba Nguvila leo Juni 27,2024 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Ilala Boma.
Akifungua mafunzo hayo Ndg Chillah amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake kwa watanzania hususani wakazi wa Mkoa huo ambapo upendo wake unajidhihirisha Katika kuhakikisha adhma ya Serikali yake ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na watoto inafanikiwa.
Katibu Tawala Msaidizi Mipango na uratibu amesema ziko jitihada nyingi ambazo zinachukuliwa na Serikali ikiwemo Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ambao umeandaliwa kwa kuunganisha Mipango Kazi tofauti nane iliyokuwa inashughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kutengeneza mpango kazi mmoja.
Aidha MTAKUWWA unalenga kutekeleza adhima ya serikali ya kutokomeza aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambazo ni ukatili wa kingono, kimwili, kihisia na kiuchumi pia Ukatili dhidi ya watoto ni matumizi ya makusudi ya nguvu au vitisho vinavyoweza kusababisha watoto kupata madhara ya kimwili, kiafya na kisaikolojia hivyo kuathiri maendeleo na utu wao.
Hivyo ametoa rai kwa wajumbe wote wa kamati ya Mkoa kufuatilia kwa makini mafunzo hayo ili kuwa mabalozi wazuri katika kufikisha ujumbe wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wajumbe wengine kama viongozi wa dini, wawakilishi kutoka Jeshi la polisi, wawakilishi wa makundi maalum ya watu wenye ulemavu, Asasi na mashirika yanayojihusisha na kupiga vita vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ambapo mafunzo hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 28,2024.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa