Mgeni Rasmi Katibu Twala Msaidizi Utawala Ndg Lawrence Malangwa akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya Siku ya wauguzi Duniani katika viwanja vya Kituo cha Afya Buza Temeke
Mkoa wa Dar es salaam Leo umeadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani ambapo wito umetolewa kwa wauguzi kuendelea kufanya Kazi kwa bidii ili kuhakikisha Wagonjwa wanapata huduma Bora za Afya.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Katibu Tawala msaidizi wa Mkoa huo, Lawrence Malangwa amesema kupungua kwa malalamiko Ya Wananchi kwenye Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati ni ishara tosha kuwa watumishi wa sekta ya Afya wanafanya kazi kubwa.
Aidha Malangwa amesema Mkoa huo utaendelea kuthamini kazi kubwa na nzuri inayofanywa na watumishi wa sekta ya Afya ambapo amewasisitiza kujiwekea utaratibu wa kukutana Mara kwa Mara ili kubadilishana uzoefu.
Hata hivyo Malangwa amesema takwimu zinaonyesha kwa siku zaidi ya watoto 500 mpaka 600 huzaliwa na wote hao wanapokelewa na mikono salama ya Wauguzi.
Maadhimisho hayo yamefanyika Viwanja vya Kituo Cha Afya Buza ambapo yameenda sambamba na Zoezi la upimaji wa magonjwa mbalimbali, uchangiaji na utoaji wa msaada vitu mbalimbali kwa Wagonjwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa