- Wananchi watakiwa kuzingatia Lishe bora kuondoa udumavu,na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza
- Waandaaji na Washiriki wa maonesho wapongezwa kwa ubunifu, na matumizi ya Sayansi na Teknolojia mpya
- Msisitizo watolewa juu Utoaji wa elimu ya lishe na uzalishaji wa chakula
Akiongea katika Maadhimisho ya kilele cha siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika leo Octoba 16,2022 katika viwanja vya Mnazimmoja Ilala Jijini Dar es Salaam Mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Kheri James ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo amewataka wananchi na wakazi wa Mkoa huo kuzingatia Lishe bora kwa kuwa Udumavu na magonjwa mengi yasiyo ambukiza yanayoikiumba jamii yanatokana na Lishe duni.
Aidha Mhe Kheri James amepongeza Waandaji na Washiriki wa maonesho hayo kwa ushirikiano waliouonyesha Kufanikisha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo yalipambwa na maonyesho ya bidhaa na huduma mbalimbali
Hata hivyo Mgeni Rasmi alivutiwa na bidhaa za kilimo, uvuvi na mifugo ambazo zimeandaliwa kwa kutumia Sayansi na Teknolojia mpya inayoendana na nyakati ya sasa.
Mhe Kheri James amewataka wananchi kutumia maonesho hayo kama nyenzo muhimu ya kujipatia elimu juu ya uzalishaji bora wenye tija wa bidhaa za kilimo, uvuvi na mifugo ili kukabiliana na ukosefu wa lishe bora na magonjwa yasiyo ambukiza katika Jamii.
Ifahamike kuwa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuzingatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu baada ya kusaini Mkataba wa Lishe tayari mkoa umejipanga kuchukua hatua za makusudi ili wananchi wapate Lishe bora yenye virutubisho vyote muhimu ikiwemo kuendelea kutoa elimu ya lishe na uzalishaji wa chakula bora
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa