Mkuu wa Mkoa Mhe Amos Makalla akifungua baraza la biashara la Mkoa wa Dar es Salaam mapema leo katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Jijijini Dar es Salaam.
# Aahidi kutekeleza mambo makuu manne (4) kwa mstakabali wa wafanya biashara wa Mkoa wa Dar es Salaam na Uchumi wa Taifa la Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla ameyasema hayo leo wakati anafungua kikao cha baraza la biashara la Mkoa wa Dar es Salaam.
Kikao cha baraza hilo la biashara la Mkoa kimefanyika katika ukumbi wa *Hotel ya Golden Tulip* Posta mpya Jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amesema Dar es Salaam ni kitovu cha kibiashara na uwekezaji na hiyo hupelekea kuwa ni Mkoa unaochangia asilimia kubwa ya pato la Taifa.
Kwa mantiki hiyo Mkoa una kila sababu ya kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa wafanyabishara na wawekezaji.
"Niwahakikishie wafanyabishara wote wakubwa na wadogo Mkoa umejiimarisha katika Ulinzi na Usalama, kukusanya kodi kwa mujibu wa sheria, kuondoa urasimu na rushwa, kujenga mahusiano mazuri na sekta binafsi wakati wote " Alisema RC MAKALLA
Aidha Mkuu wa Mkoa amefafanua katika kuondoa urasimu na rushwa mkoa umeanzisha "One Stop Centre" ambayo ndani yake kutakuwa na taasisi anuai kama vile TRA, BRELLA OSHA, TBS, TMDA nk, na hilo linaanza rasmi 1/09/ 2021 na itakuwa chini ya ofisi ya Mkuu Mkoa na badae itashuka chini katika ngazi za Wilaya.
Vilevile amesema Dar es Salaam lazima iwe safi na mpangilio mzuri wa wafanyabiashara wadogo mpango wa utekelezaji wa jambo hilo unakuja hivi karibuni.
Aidha kwa kuwa Taifa linapitia wimbi la tatu la ugonjwa wa UVIKO-19 Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Rashid Mfaume ameendelea kutoa rai kwa jamii kuendelea kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huo kupitia mwongozo wa Wizara ya Afya na amehimiza umuhimu wa chanjo na vituo vya kuotoa chanjo vipo katika Mkoa Jamii itumie vizuri fursa hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa