Kufuatia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 28/10/2020 wa kuchagua Madiwani, Wabunge na Rais , Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefungua rasmi mafunzo ya siku tatu (3) kwa wasimamizi ya Uchaguzi kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, mafunzo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakila kiapo wakati wa ufunguzi wa semina hiyo katika ukumbi wa chuo cha utalii Jijini Dar es Salaam
Akifungua mafunzo hayo kamishina wa Tume ya Uchaguzi Bi Asina Omary amesema mafunzo hayo yamelenga hasa kuelekezana, kujadili, na kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kufanikisha shughuli hiyo kubwa ya kitaifa kwa kufuata sheria,kanuni,na taratibu za uchaguzi kwa kuwa ni takwa la kikatiba.
Aidha kamishina wa Tume ya Uchaguzi amewataka washiriki wote wa mafunzo kuhakikisha wanakuwa wasikivu waepuke kufanya kazi kwa mazoea, kikubwa zaidi wazingatie maadili ya uchaguzi, sheria,kanuni na taratika za kikatiba zinaongoza uchaguzi mkuu.
Ni muhimu pia kwa kila msimamizi wa uchaguzi kutambua maeneo yake ya kufanyia kazi ikiwemo miundombinu ya kufika katika kata na vituo vya kufanyia uchaguzi sambamba na maeneo ya kufanyia mafunzo ya uchaguzi.
Lakini pia ametoa rai kwa waratibu na wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha yafuatayo hayatokei katika kipindi cha zoezi hilo la uchaguzi kama vile kuweka meza,viti nk katika kituo cha uchaguzi siku ya uchaguzi asubuhi, kuchelewa kufungua vituo vya uchaguzi ikimaanisha kufungua kituo muda tofauti na uliowekwa na Tume.
Lakini pia kuhakikisha katika kila kituo watendaji wanavifaa vyote vinavyohitajika katika shughuli nzima ya uchaguzi, aidha watendaji watakaoshughulika na kazi hiyo wawe ni watu wenye weledi,kujiamini na uwajibikaji ili kuwezesha zoezi hilo kufanyika kwa mafanikio makubwa.
Aidha mafunzo ya watendaji katika vituo vya uchaguzi yafanyike kwa ufanisi mkubwa ukizingatia wao ndio watakaotekeleza zoezi hilo na kuwezesha kufanikisha kwa uchaguzi pasipo malalamiko sambamba na kufuata utaratibu wa kuweka mawakala wa vyama vya siasa .
Mwisho kamishina wa uchaguzi amehimiza umuhimu wa kuwa na maghala yenye ulinzi wa kutosha tayari kwa kupokea vifaa vya uchaguzi, na kwa kila mtendaji katika zoezi hilo anapaswa kujiamini,kujitambua na kuzingatia misingi ya kikatiba,sheria, na taratibu za uchaguzi mkuu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa