- Ampongeza RC MAKALLA kwa Uongozi mzuri wa utekelezaji wa Oparesheni hiyo
-Ataja Takwimu za Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam
-Asisitiza kuwa zoezi hili ni endelevu, Majina ya Mitaa yaamuliwe na wenye Mitaa Yao na Maeneo yenye Migogoro yatafikiwa baada ya Migogoro hiyo kuisha
-Naibu Waziri OR- TAMISEMI David Silinde Aagiza kabla ya Mei 30 2022 Oparesheni hii ikamilike
-RC Makalla asema Dsm imekamilisha Oparesheni hii na hakuna Halmashauri iliyochini ya Asilimia 100
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye leo tarehe 18 Mei 2022 amefanya ziara ya Kukagua utekelezaji wa Oparesheni Kabambe ya Anwani za Makazi na Postikodi katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amepongeza na kusema Mkoa wa Dar es Salaam Umefanya Vizuri Sana katika Oparesheni hiyo
Waziri Nape amempongeza pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla kwa Uongozi wake mzuri ambapo amewaelekeza, amewaagiza, amewashirikisha na kuwaongoza vema Wakuu wote wa Wilaya katika Mkoa wake hatimae matunda yake leo yanaonekana
Hata hivyo Waziri Nape ametaja Takwimu zilizofikiwa katika Mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni Ilala Asilimia 113, Kinondoni 103.17, Temeke 102.24, Ubungo 101.97, na Kigamboni 118.55
Vilevile Mhe. Nape amesisitiza kuwa zoezi hili ni endelevu ili kukidhi Mahitaji ya nyumba zinazoendelea kujengwa, majina ya Mitaa yaamuliwe na wenye mitaa husika ili kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza na maeneo yenye migogoro mbalimbali yatafikiwa baada ya migogoro Yao kuisha
Kwa upande wa Naibu Waziri wa OR- TAMISEMI David Silinde ameagiza Oparesheni hii kukamilika kabla ya Mei 30, 2022 na kuwataka kila Mtendaji kutimiza wajibu wake
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amesema Dar es Salaam imekamilisha Oparesheni hii na hakuna Halmashauri iliyo chini ya Asilimia 100 hivyo maeneo sasa yatafikika na Tanzania itasomeka Duniani
#KESHO YAKO NI ANWANI YA MAKAZI#
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa