- Wito watolewa Kwa Wazazi kuhakikisha watoto wao wanapatiwa Chanjo.
- Walengwa ni watoto Wenye Umri wa Chini ya miaka 5.
- Zaidi ya Watoto laki Tisa wanategemewa kuchanjwa.
Mkoa wa Dar es salaam unataraji kufanya Kampeni ya utoaji wa Chanjo ya matone ya kuzuia ugonjwa wa kupooza ghafla (Polio) ambapo wito umetolewa kwa Wazazi kuhakikisha watoto wao wanapatiwa Chanjo hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dr. Rashid Mfaume amesema zoezi Hilo litaanza Alhamis ya September 01 mpaka Jumapil ya September 04 ambapo zaidi ya watoto laki Tisa wanatarajiwa kupata Chanjo hiyo.
Aidha Dr. Mfaume amesema tayari timu 2,042 za wataalamu wamejipanga kupita nyumba kwa nyumba kutoa Chanjo ambapo Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano.
Hata hivyo Dr. Mfaume amesema kwa Wazazi ambao watoto wao walishapata Chanjo kipindi Cha hivi karibuni haizuii kupata Chanjo itakayotolewa Sasa kwakuwa itazidi kuimarisha Afya Zaidi.
Chanjo ya polio itatolewa kwa Watoto wa Chini ya miaka 5 ambapo Baada ya mtoto kuchanjwa atapakwa wino maalumu kwenye kidole na nyumba kuwekwa alama ya Tick kwa kutumia chaki kwenye mlango ambapo timu ya Afya Mkoa watafanya ufuatiliaji wa zoezi Hilo katika Halmashauri za Mkoa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa