- Apongeza Kampeni ya Usafi, Kuwapanga vizuri Wamachinga na Uratibu mzuri wa Bodaboda Wenye ulemavu DSM
- Akiri kazi inayofanyika ya kuongoza Jiji kubwa kama DSM sio ndogo na RC MAKALLA ameweza
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Comred Daniel Chongolo amemwagia Sifa za utendaji Kazi uliotukuka RC Makalla katika Jiji kubwa la Dar es Salaam.
Comred chongolo amesema Jiji la Dar es Salaam sasa ni SAFI Kampeni za Usafi zinaendelea, Wamachinga wamepangwa vizuri Hongera sana Kamisaa Amos Makalla
Aidha Mhe Chongolo amesema anafurahishwa sana na zoezi linaloendelea sasa la kuratibu vizuri Bodaboda na Wenye ulemavu katika Jiji la DSM ili waweze kujipatia riziki, ijapokuwa kuna upotoshaji na maneno maneno yanayoendelea.
"Niwahakikishie nimefuatilia kwa makini madai ya zuio la Boda boda katika Jiji la DSM, ukweli ni kwamba kinachofanyika ni kuwaratibu vizuri Bodaboda na Wenye Ulemavu kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwa na vituo rasmi ili kuweza kuwasimamia vizuri, tuache kupotosha" Alisema Comred Chongolo
Comred Chongolo amesisitiza kazi ya Katibu wa Chama ni mtendaji mkuu wa shughuli za chama na anawajibika kufuatilia Utekelezaji wa Ilani, hivyo haiwezekani kufumbia macho Bodaboda ambao ni kundi kubwa na muhimu ambalo limejiajili ili kujipatia riziki pasipo kuwawekea mazingira mazuri hivyo kinachofanyika Jiji la Dar es Salaam kwa Bodaboda na Wenye Ulemavu ni Cha kupongezwa Hongereni sana.
Mhe Daniel Chongolo amekiri Jiji la DSM ni kubwa kuliongoza na mambo yakaonekana ni kazi kubwa amempongeza sana RC Makalla huku akibainisha kuwa CCM inatambua kazi nzuri inayofanywa.
Ifahamike kuwa Pongezi hizo zimetolewa na Comred Daniel Chongolo mapema leo wakati akihitimisha Ziara yake ya kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM- DSM katika Ukumbi wa Mikutano Anatoglo Mnazimmoja Ilala Jijini Dar es Salaam
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa