Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam leo Novemba 27,2023 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya barabara inavyotekeleza na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini TARURA katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo ikiwemo Barabara ya Kinzudi- Goba Wilaya ya Ubungo, Jamirex-Mwenge Wilaya ya Kinondoni na Chanika Homboza Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa ziara hiyo kwa niaba ya CCM Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa Mhe Abbas Mtevu amesema Chama kimeridhishwa namna Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini TARURA inavyotekeleza ujenzi wa miundombinu ya Barabara katika Mkoa huo ambapo ametoa maelekezo kwa TARURA kujipanga vizuri katika ukarabati wa barabara pindi zinapokuwa na mashimo na kuzikarabati mapema kabla hazijaharibika zaidi.
Kwa Upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amesema maeneo ambayo yana Changamoto kubwa za Barabara katika Mkoa huo ni Wilaya ya Ubungo na Kigamboni lakini Mhe Rais Dkt Samia tayari ameshaidhinisha pesa kupitia DMDP awamu ya pili ambazo zinakwenda kupunguza Changamoto za Barabara kwa kiwango kikubwa katika Wilaya hizo.
Aidha Mhe Albert Chalamila amesema katika kukabiliana na uharibifu wa miundombinu unaotokana na mvua zinazoendelea kunyesha tayari Mkoa umejipanga kujenga miundombinu hiyo mara tu mvua zikiisha ili kuepuka hasara zisizo za lazima labda tu kwa eneo ambalo litaonekana kuwa na ulazima nyakati za mvua Mkoa utafanya hivyo " Vilevile Ujenzi utakofanyika sasa lazima uakisi mabadiliko ya tabia ya nchi" Alisema RC Chalamila.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini TARURA Mkoa huo Mhandisi Godfrey Mkinga amesema TARURA inasimamia Mtandao wa Barabara wenye jumla ya urefu wa Kilometa 5,059.05, mtandao umegawanyika katika sehemu kuu tatu, Barabara za Mlisho (feedders), Barabara za Mkusanyo (Collector) na Barabara za Jamii (Community) ambapo amesema kati ya hizo urefu wa Kilometa 610.69 ni barabara za Lami/Zege, Kilometa 1,642.90 ni barabara za changarawe, na Kilometa 2,805.48 ni barabara za udongo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa