- RC Chalamila atangaza Operesheni kali kuendelea maeneo yote ambayo bidhaa hizo hupitishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 11, 2024 ametangaza kuendelea kwa Operesheni kali ya kudhibiti upitishwaji holela wa bidhaa mbalimbali za magendo katika fukwe za bahari ya Hindi ambapo amesema yoyote atakaye kamatwa adhabu kali itachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za nchi.
RC Chalamila amebainisha bidhaa za magendo zilizokamatwa ni mifuko ya sukari zaidi ya 100, madumu ya mafuta ya kupikia zaidi ya 700 pamoja watuhumiwa zaidi ya 7 ambapo ameagiza watuhumiwa wote wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Aidha RC Chalamila amesema bidhaa hizo zilizokamatwa zimetoka upande wa Zanzibar kuja Tanzania bara kwa kutumia mashua " Kushamiri kwa uingizaji wa bidhaa za magendo ni kulikosesha Taifa mapato lakini pia ni hatari kwa afya za binadamu kwa kuwa bidhaa hizo zinakuwa hazija pimwa ubora" Alisisitiza RC Chalamila
Vilevile RC Chalamila amesema lazima tulinde kama tulivyo kula kiapo hatuwezi kuruhusu magendo katika Mkoa huu tuko imara sana kwa masilahi mapana ya ustawi wa jamii na amani ya Taifa hili
Ifahamike kuwa bidhaa hizo za magendo zimekamatwa usiku wa kuamkia jana Februari 10 kupitia kikosi kazi cha kudhibiti mtandao mzima wa upitishwaji wa bidhaa za magendo katika fukwe za bahari ya Hindi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa