- Asema Waratibu wa majukwaa wawe chachu ya kuibua vitu tofauti vya kujifunza
- Awataka wananawake katika majukwaa kujikita katika Uzalishaji kwa kuwa hukuza Uchumi
-Asisitiza DSM ni Jiji la Kibiashara ataka majukwaa yawe ya mfano wengine waje kujifunza
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi Beng'i Issa ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya ushirika wa viwanda kwa viongozi wa Jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Mkoa wa Dar es Salaam mafunzo ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Tirdo Wilaya ya Kinondoni- Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa NEEC amesema majukwaa hutoa fursa kwa wanawake kukutana na kujadili masuala ya Biashara na Uchumi hivyo Waratibu wa majukwaa hayo wanatakiwa kuwa wabunifu na kuibua vitu tofauti vya kujifunza itasaidia kuwajengea uwezo ambao utaleta tija kwa mfano Mafunzo ya leo tayari wanawake wameelewa dhana ya madirisha na namna inavyoweza kuwasaidia kujikwamua Kiuchumi.
Aidha Bi Beng'i Issa amewataka wanawake katika Majukwaa kujikita katika Uzalishaji huku akiwahakikishia ukizalisha katika viwango masoko sio tatizo, lakini ni vizuri kazi hizo zikafanywa kwa kushirikiana, ushirika ndio unaweza kuwainua kinachotakiwa ni kuwa na namna bora ya ushirikiano.
Hata hivyo amepongeza namna Mkoa wa Dar es Salaam unavyofanya ubunifu katika kuendesha Jukwaa la Kuwezesha Wananchi Kiuchumi amewataka kuwa wabunifu zaidi, Dar es Salaam ndio jiji la Kibiashara kuna fursa kubwa ya kufanya vizuri na mikoa mingine ya Tanzania ije kujifunza.
Bi Beng'i Issa ametoa rai hususani kwenye Suala la Mitaji ni vizuri kuwa na utaratibu wa kuweka kumbukumbu za biashara ili taasisi za fedha ziweze kuwakopesha
Kwa Upande wa Mratibu wa Jukwaa la kuwezesha Wananchi Kiuchumi Mkoa wa Dar es Salaam Bi Zubeda Masoud amesema Jukwaa hilo liko imara toka kuanzishwa kwake limeendelea kuimarika ni imani yake kuwa litakuwa la mfano Mikoa mingine waje kujifunza katika Jukwaa hilo.
Afisa Masoko na Uhusiano UTT, Bwana Waziri Ramadhani akitoa darasa kwa wanawake viongozi wa Jukwaa la kuwezesha Wanawake kiuchumi Mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Tirdo Msasani- Kinondoni
Mratibu wa Jukwaa la Kuwezesha Wananchi Kiuchumi Mkoa wa Dar es Salaam Bi Zubeda Masoud aliyesimama akiongea wakati wa mafunzo hayo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa