Hayo yamesemwa leo Desemba 14, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert John Chalamila wakati akizungumza na askari kwenye ukumbi wa Polisi wa Barracks uliopo wilayani Temeke - DSM.
RC Chalamila alisema vyombo vya dola vinapata sifa pale askari wanapokuwa waadilifu wakiwa wanatekeleza majukumu katika kusimamia haki, ulinzi, amani na usalama wa raia na mali zao kwa kuzingatia misingi ya utumishi wa umma " kamwe usikubali kufanya jambo lolote linalodharirisha Jeshi la polisi au heshima na utu wako" Alisisitiza RC Chalamila
Aidha RC Chalamila amewataka askari hao wafanye kazi kwa kushirikiana wao wenyewe na raia, na wawe mstari wa mbele na viongozi na katika kutatua matatizo na changamoto kabla hazijawa sugu.
"Endapo wasipotatua tatizo, tatizo litazidi kukua na likishakua ndilo litachukua nafasi ya uongozi ndipo kiongozi ataonekana tatizo kwenye jamii husika kwasababu ameshindwa kujiamini ili kutatua tatizo hivyo, simameni kama viongozi wakati wakutatua changamoto mbalimbali
Vilevile RC Chalamila amewaasa kuepukana vitendo vya rushwa na kuielewa vizuri dhana ya uadilifu na umasikini, utakuta mtaani wanasema we kuwa muadilifu ufe masikini hiyo sio kweli unauwezo wa kuwa tajiri ndani ya uadilifu. ni vizuri uwe kiongozi unayejitambua mwenye kuisemea vizuri serikali na nchi ya Tanzania.
"Tunaelekea kwenye kipindi cha uchaguzi Mwaka 2024/2025 ni mahala pazuri pa kushirikiana katika kufanya kazi ya kuhakikisha Mkoa na nchi inakuwa na amani kwa kuweka mikakati endelevu ya pamoja ya kulinda amani ya nchi kwa kuzingatia haki za wananchi pamoja na kutowavumilia watu wanaopanga au wanaofanya uharifu.
Mwisho Mhe Mkuu wa Mkoa amesema anafurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na Jeshi hilo Katika Mkoa wa Dar es Salaam, anajivuni kuwa na Jeshi hilo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa