Kiongozi wa Waislamu wa Dhehebu la Ismaili Duniani Mtukufu Aga Khan amehitimisha ziara yake ya siku mbili Nchini kwa Mwaliko wa Rais Dr. John Magufuli ambapo ameagwa na Waziri wa Ulinzi Dr. Hussein Mwinyi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ni miongoni mwa Viongozi waliomsindikiza Mtukufu Aga Khan ambapo amesema ujio wa Kiongozi huyo umekuwa fursa kubwa kwa Taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, Uchumi na sekta nyingine.
Amesema kuwa Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Mtukufu Aga Khan kwenye Hospital, Shule na Hotel umekuwa na Tija kwa Taifa katika kutoa fursa za Ajira.
Wakati Mtukufu Aga Khan anaondoka Uwanja wa Ndege alimuuliza RC Makonda kitu gani anataka afanyiwe kwenye Mkoa wake ndipo RC Makonda akamuelezea Kampeni ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu ambapo Aga Khan amepokea kwa Asilimia mia moja na kutoa maelekezo kwa wasaidizi wake Nchini kumuunga mkono ambapo wameahidi kukabidhi Mchango wao kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa hivi karibuni.
Amempongeza Rais Dr.Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya inayopelekea Viongozi wakubwa ulimwenguni kuja Nchini mara kwa mara.
Itakumbukwa kuwa hata kwenye kampeni ya upimaji wa Afya bure moja ya Hospital zilizojitolea kumuunga mkono ni pamoja na Aga Khan
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa