Wednesday 1st, January 2025
@Viwanja vya Jakaya M. Kikwete Youth Park
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila Mwaka tarehe 16 Juni baada ya kupitishwa kwa Azimio la nchi 51 wanachama wa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU). Tanzania kama nchi mwanachama wa Umoja wa Umoja wa Afrika imekuwa ikiadhimisha siku hii tangu mwaka 1991. Lengo la kuadhimisha siku hii ni kukumbuka mauaji ya kinyama waliyofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mwaka 1976.
Katika ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam Maadhimisho haya yatafanyika katika Viwanja vya Jakaya M. Kikwete Youth Park (JMK Park),kidongo chekundu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni.
KAULI MBIU
Kauli mbiu ya mwaka huu 2017 ni "Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa sawa kwa watoto."
Wananchi wote mnakaribishwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa