Wednesday 1st, January 2025
@Uwanja wa Jamhuri - Dodoma
YALIYOJIRI LEO NOVEMBA 24, 2017 KATIKA MAHOJIANO MAALUMU NA WAZIRI WA NCHI - OFISI YA WAZIRI MKUU, JENISTA MHAGAMA KUHUSU MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA UHURU.
#Nchi yetu itaadhimisha sherehe ya kutimiza miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara mnamo Disemba 9 mwaka huu - Waziri Jenista Mhagama.
#Maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma -Waziri Jenista Mhagama.
#Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli - Waziri Jenista Mhagama.
#Shughuli zinazotarajiwa kufanyika siku hiyo ni maonesho ya gwaride la heshima lililoandaliwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama nchini - Waziri Jenista Mhagama.
#Shughuli zingine ni onesho la Kikosi cha makomando na kwata ya kimyakimya kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania - Waziri Jenista Mhagama.
#Kutakuwa na onesho la Gwaride la Mkoloni kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Gwaride la wanafunzi wa shule za Sekondari Dodoma - Waziri Jenista Mhagama.
#Itakuwa ni mara ya kwanza Onesho la Gwaride la Mkoloni kufanyika Tanzania Bara - Waziri Jenista Mhagama.
#Vile vile kutakuwa na burudani za vikundi vya ngoma za asili kutoka Ruvuma, Kigoma na Zanzibar pamoja na vikundi vya kwaya kutoka Chunya, Mbeya - Waziri Jenista Mhagama.
#Pia kutakuwa na burudani ya muziki wa kizazi kipya ikiwemo kikundi cha Tanzania All Stars - Waziri Jenista Mhagama.
#Kauli mbiu ys sherehe hizi ni "UHURU WETU NI TUNU: TUUDUMISHE, TULINDE RASILIMALI ZETU, TUWE WAZALENDO,TUKEMEE RUSHWA NA UZEMBE". - Waziri Jenista Mhagama.
#Natoa wito kwa wananchi wote kusheherekea siku hii kwa kudumisha amani, upendo,umoja na mshikamano kwa maendeleo ya nchi yetu - Waziri Jenista Mhagama.
#Maadhimisho hayo yataanza saa 12:00 asubuhi hivyo nachukua nafasi hii kuwakaribisha wananchi wa Dodoma na mikoa ya karibu kujitokeza kwa wingi kusherehekea kwa pamoja kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu - Waziri Jenista Mhagama.
IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI - MAELEZO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa