Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda anawakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kushiriki katika kuuaga Mwenge wetu wa Uhuru kesho saa 1:30 asubuhi katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal one.
Ikumbukwe kuwa Mwenge wetu wa Uhuru ulipokelewa kutoka katika Mkoa wa Lindi tarehe 27/05/2017 na kukagua miradi mbalimbali yenye thamani ya Tshs 244,392,530,334/= katika mkoa wetu kwa muda wa siku tano ambapo shughuli za kuzindua miradi mikubwa 12 zilifanyika ,miradi 5 ikiwekewa mawe ya msingi, na miradi 11 ikitembelewa na kufunguliwa.
Wakazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam tujitokeze kwa wingi kuuaga Mwenge wetu wa Uhuru.
Imetolewa na:-
Kitengo cha Habari na Uhusiano
OFISI YA MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM
31/05/2017
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa