HALI YA UTOAJI HUDUMA YA MAJISAFI, UONDOAJI MAJITAKA NA
MIPANGO ILIYOPO NA MIRADI INAYOEENDELEA
MKOA WA DAR ES SALAAM
HADI JUNI, 2018
HUDUMA YA MAJI
Mahitaji ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam hadi mwezi Juni, 2018 ni wastani wa lita milioni 544 kwa siku ambapo uwezo wa uzalishaji ni lita milioni 502 kwa siku. Vyanzo vikuu vya maji haya ni Mto Ruvu (88%), Mto Kizinga (03%) na visima virefu (09%). Maji yanayozalishwa kwa sasa yanakidhi mahitaji kwa asilimia 75 ya wakazi wa Jiji. Takriban asilimia 40 ya eneo la Mkoa halina mtandao wa mabomba ya DAWASA ambapo huduma hupatikana kupitia Visima vya Taasisi na watu binafsi, huduma hii huchangia asilimia 16 ya mahitaji.
Maeneo machache (20%) yaliyopo hasa katika Wilaya ya Kinondoni, Ilala na Ubungo hupata huduma ya maji kwa saa kati ya 20-24 wakati zaidi ya asilimia 40 hupata maji kwa mgawo wa wastani wa saa kati ya 8-16 kwa siku.
Eneo kubwa la Wilaya za Temeke na Kigamboni ndilo lenye kiwango cha chini ya asilimia 10 ya upatikanaji wa mtandao wa mabomba. Maeneo haya yanatarajiwa kupata huduma ya maji kutoka mradi mkubwa unaoendelea hivi sasa wa visima virefu 20 vya Kimbiji na Mpera
Jitihada za kuongeza mtandao wa Majisafi zinaendelea ili watu wengi zaidi waweze kunufaika. Hadi kufikia mwezi Juni, 2018 asilimia 75 ya wakazi waishio kwenye Mitaa katika Mkoa wa Dar es Salaam wanapata huduma ya majisafi na salama kupitia miradi ya maji iliyopo.
1.2 Hali ya Uondoshaji Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam
Mfumo (Central sewerage system) wa kuondosha Majitaka uliopo Jijini Dar es Salaam unahudumia asilimia 10 tu ya wakazi wote wa Jiji. Mifumo mingine ipo Lugalo, Chuo Kikuu cha DSM, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Kurasini, Buguruni, Uwanja wa Ndege, Airwing, Barabara ya Nyerere (Tazara), Vingunguti na Ubungo. Mifumo hii inamwaga majitaka katika mabwawa yaliyoko maeneo hayo.
Maeneo yasiyo na mfumo rasmi wanatumia vyoo vya shimo (Pit latrine) asilimia 70 na mashimo ya choo (septic tanks) asilimia 20.
Matarajio ya Mkoa ni kutoa huduma ya Majisafi na salama kwa asilimia 95 ya wakazi wa Jiji na asilimia 30 uondoshaji wa Majitaka katika Mkoa wa Dar es Salaam ifikapo 2025.
Hivi sasa Mkoa wa Dar es Salaam unaendelea kutekeleza jumla ya miradi 18 kati ya 41 ya visima vya maji iliyopangwa, katika Manispaa ya Ilala, Kigamboni, Kinondoni, Temeke na Ubungo chini ya mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Maji. Kati ya miradi hiyo, 10 imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi (Pugu Kajiungeni, Kipunguni B, Makongo Mbuyuni, Kivule, Goroka, Mianzini, Kizinga Bughidad, Mashine ya Maji, Kibwegere na Mpiji-Magohe). Aidha, miradi 3 ya Mbuyuni, Mamboleo B na Mabatini ipo katika hatua ya majaribio ya utoaji wa huduma ya maji. Kazi za utekelezaji wa miradi 5 ya maji ya Chambewa, Kibene, Malimbika, Kizuiani na Mbezi Makabe zinaendelea.
Katika kuhakikisha miradi ya maji inakuwa endelevu, miradi yote inaendeshwa na wananchi wenyewe kupitia Vyombo vya Watumiaji Maji/Vikundi vinavyoundwa kisheria. Aidha, miradi ambayo inatumia mtandao wa DAWASA uendeshaji wake unakuwa chini ya DAWASCO.
1.3.2 Miradi Mingine inayotekelezwa kwenye Halmashauri
Kupitia bajeti za Halmashauri (Own Source, UNICEF, LGCGD, BTC, WATER AID, Africa Relief, Food Aid Counterpart na mfuko wa Jimbo) Halmashauri zote tano zinaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji katika maeneo yao kama ifuatavyo:-
Manispaa ya Ilala
Katika Manispaa ya Ilala, jumla ya Miradi 10 inatekelezwa katika maeneo ya Pugu Bangulo, Kinyerezi, Pugu Kichangani, Ulongoni A, Lada, Lubakaya, Lukooni, Segerea, Kitonga. Upanuzi wa mradi wa usambazaji wa maji katika maeneo ya Kinyamwezi, Mustafa na Viwege ujenzi wake umekamilika. Wananchi 27,064 wananufaika na huduma ya maji inayotolewa katika maeneo hayo. Aidha, Mradi wa maji katika mtaa wa Mkera ujenzi wake unaendelea na umefika asilimia 90.
Manispaa ya Kigamboni
Manispaa ya Kigamboni kuna jumla ya Miradi 2, mradi wa Mwasonga-Kisarawe II ujenzi wake umekamilika na umeanza kutoa huduma ya majaribio na Minondo Somangila ambao ujenzi umesimama kwa muda kupitisha nguzo za umeme.
Manispaa ya Kinondoni
Jumla ya Miradi 3 ya Makongo Juu, Kigogo Buyuni na Shule ya Msingi Changanyikeni imekamilika. Wananchi 7,017 wananufaika na huduma ya maji inayotolewa.
Mradi wa maji wa Mivumoni ukarabati wake unaendelea, ununuzi wa Pampu mpya unahitajika baada ya ile ya awali kuharibika.
Manispaa ya Temeke
Manispaa ya Temeke, jumla ya Miradi 3 ya Kurasini-Mvinjeni, Buza na Makuka ujenzi wake umekamilika na imeanza kutoa huduma ya maji. Wananachi zaidi ya 7000 wananufaika na mradi
Mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika kata tatu maeneo ya Kibondemaji unaotekelezwa kwa msaada wa Shirika la Water Aid/PDF ujenzi wake umekamilika na umeanza kutoa huduma kwa jamii. Mradi unahudumia Wananchi 19,500.
Mradi wa Maji wa Mkondogwa unaendelea na ujenzi wake upo hatua za mwisho za ukamilishaji.
Ujenzi wa mfumo wa kutibu Majitaka (DEWATs) katika eneo la Toangoma unaotekelezwa kwa msaada wa Shirika la Water Aid/PDF, ujenzi wake unaendelea ambapo hadi sasa umefikia 98%, kazi zilizobaki ni ujenzi wa fensi na kusawazisha eneo.
Manispaa ya Ubungo
Jumla ya Miradi 4 ya Makurumla mnara wa Voda, Makurumula Sisi kwa Sisi, Nzasa A na King'azi imekamilika na inatoa huduma kwa Wananchi 11,100.
Upanuzi wa mradi wa King’azi A unaendelea, ukihusisha ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa uwezo wa lita 90,000 litakalohudumia wakazi wapatao 15,400. Hadi sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 40.
Ujenzi wa mfumo wa kutibu Majitaka (DEWATs) katika eneo la Mburahati/ Barafu, umefikia asilimia 60 ya utekelezaji.
Maelezo ya kina kuhusu mipango iliyopo na miradi mbalimbali inayoendelea yanapatikana kwenye Jedwali Na I.
1.3.3 Miradi Inayoteekelezwa na DAWASA
i)Upanuzi wa Mtambo wa Ruvu Chini na ujenzi wa bomba kuu kutoka Ruvu Chini hadi matanki ya Chuo Kikuu cha Ardhi.
Lengo la mradi huu ni kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 182 hadi 270 kwa siku. Mradi wa upanuzi wa mtambo umekamilika kwa asilimia 100 na unatoa huduma. Mradi huu umepunguza kero ya maji kwa wakazi wa maeneo ya Bunju, Mabwepande, Boko, Tegeta, Kunduchi, Mbezi Beach, Mbezi Juu, Salasala, Kawe, Makongo, Chuo Kikuu, Mikocheni, Msasani, Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Sinza, Manzese, Ubungo, Mabibo, Kigogo, Buguruni, Ilala, Maeneo ya Katikati ya Jiji la DSM pamoja na Kurasini, Keko, Chang'ombe, Pugu Road na Bandarini.
ii) Upanuzi wa chanzo cha Ruvu Juu na ujenzi wa bomba kuu hadi matanki ya Kibamba na Kimara.
Lengo la mradi huu ni kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 82 hadi 196 kwa siku. Upanuzi wa mtambo umekamilika kwa asilimia 100. Kukamilika kwa mradi huu kumepunguza kero na uhaba wa maji katika maeneo Kiluvya, Kibamba, Changanyikeni, Ubungo, Mbezi, Makabe, Msakuzi, Malamba Mawili, Matosa, Kimara, Kibangu, Makuburi, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Vingunguti, Airport, Ukonga, Kipawa na katikati ya Jiji la DSM.
iii)Mradi wa visima virefu 20 Kimbiji na Mpera na Uchimbaji wa Visima vya Majaribio.
Lengo la mradi ni kuzalisha lita milioni 260 za maji kwa siku. Kazi ya uchimbaji visima 19 kati ya 20 unaendelea ambapo visima 14 vimechimbwa hadi mwisho, wakati visima 05 uchimbaji wake unaendelea.
Visima vya maeneo ya Mpera vitahudumia wakazi wa maeneo ya Gongo la Mboto, Chanika, Luzando, Pugu, Mpera, Chamazi, Kitunda, Ukonga, Kinyerezi, na Uwanja wa Ndege;
Visima vya maeneo ya Kimbiji vitahudumia wakazi wa maeneo ya Temeke, Kisarawe, Kibada, Kimbiji, Kigamboni, Tuangoma, Mkuranga, Kongowe, Mbagala, Kurasini, Mtoni, Tandika, Keko na Chang’ombe. Mradi wa uchimbaji visima unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwaka huu 2018. Aidha, Mradi wa uendelelezaji mradi huu upo katika hatua za majadiliano.
Mradi wa Upanuzi wa Mfumo wa Kusambaza majisafi.
Lengo la mradi ni kuongeza mfumo wa usambazaji maji na kuunganisha wateja wote walioko katika maeneo yasiyo na mtandao na yale yatakayopata maji kutokana na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Chini na Ruvu Juu, pia maeneo yatakayopata maji ya visima vya Kimbiji na Mpera. Mradi huu unaendelea kwa maeneo yanayopata maji kutoka mitambo ya Ruvu. Maelezo ya kina kuhusu mipango iliyopo na miradi mbalimbali inayoendelea yanapatikana kwenye Jedwali Na II.
2.0 MAFANIKIO
Kukamilika kwa Mradi Mkubwa wa Ruvu Chini ambao umeongeza upatikanaji wa Maji kutoka Lita Milioni 182 na kufikia lita milioni 270. Mradi umekamilika Mwezi Machi, 2016 na unatoa huduma ya maji kwa Wananchi;
Kukamilika kwa Mradi Mkubwa wa Ruvu Juu ambao umeongeza upatikanaji wa Maji kutoka Lita Milioni 82 na kufikia lita milioni 196. Mradi umekamilika Mwezi Aprili, 2017na unatoa huduma ya maji kwa Wananchi;
Kuendelea na uchimbaji wa visima 20 vya Kimbiji na Mpera ambavyo vitaongeza upatikanaji wa maji kwa lita milioni 260;
Kukamilika kwa miradi ya Visima 15 vya ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji (BTC) ambayo inahudumia zaidi watu 250,000;
Kukamilika kwa miradi ya visima 10 vya mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Maji (BRN) ambayo inahudumia zaidi watu 120,000;
Kukamilika kwa miradi ya visima vya dharura vya DAWASA, Mapato ya ndani ya Manispaa, Mfuko wa Jimbo, Water Aid,TASAF,African Relief of Kuwait na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo inahudumia zaidi ya watu 230,000.
Matarajio ya Mkoa ni kuwapatia watu huduma ya Majisafi kwa asilimia 95 ya wakazi wote na uondoshaji wa Majitaka kwa asilimia 30 ifikapo mwezi Desemba 2025.
Changamoto kubwa katika utoaji wahuduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam ni kasi ndogo ya uwekezaji ukilinganishwa na kasi kubwa ya ongezeko la watu. Ongezeko kubwa la watu Jijini hasa kuanzia miaka ya 1980 kwa kiasi kikubwa limechangia katika kuongeza mahitaji ya maji. Changamoto zingine ni pamoja na:-
S/No
|
CHANGAMOTO
|
MIKAKATI
|
1
|
Upanuzi wa mtandao wa DAWASA kutokukidhi ya mahitaji wa wakazi wa Jiji
|
Mtandao wa kusambaza maji kutoka visima 20 vya Kimbiji na Mpera ujengwe
|
2
|
Upatikanaji wa maeneo ya
kujenga miundombinu |
Kuendelea kuwasiliana na Wadau ili kupata maeneo ya kujenga miundombinu ya maji na pia kutumia way leave zilizopo kwa kukubaliana na Taasisi husika
|
4
|
Ukuaji na ujenzi holela wa
makazi, |
Ushirikishwaji wa Jiji, Manispaa na Wizara ya Ardhi katika Upangaji wa Miji.
|
5
|
Wizi wa maji, uharibifu na wizi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka,
unachangia kiwango kikubwa cha maji yasiyolipiwa |
Kushirikiana na wananchi, vyombo vya ulinzi na usalama katika kulinda miundombinu na kuzuia wizi wa maji na uharibifu wa miundombinu na uchafuzi wa maji.
|
6
|
Watumiaji maji kutokulipa
Ankara za maji kwa wakati, |
Kuweka dira za maji kwa wateja wote, usomaji wa dira za maji kufanywa kwa kutumia vifaaa maalum vya kuchukua kumbukumbu (data loggers) ili kupata takwimu sahihi.
|
7
|
Gharama kubwa za uendeshaji ikilinganishwa
na makusanyo, |
Gharama za maji ziende sambamba na Gharama za uzalishaji maji pamoja na uwekezaji;
|
8
|
Mfumo wa kuondoa majitaka haujafika maeneo mengi ya Jiji (unakidhi asilimia 10 tu)
|
|
9
|
Ufinyu wa bajeti/kuchelewa kutolewa fedha za kutekeleza miradi mipya ya maendeleo
|
Serikali inaendelea na utafutaji fedha kutoka kwa Wadau wa Maendeleo na kutenga kwenye bajeti kwa ajili ya Utekelezaji miradi mikubwa.
|
10
|
Migogoro ya uendeshaji Miradi ya Maji ya Jamii inayosimamiwa na Jumuia za Watumia Maji (COWSOs).
|
Tathmini imefanyika kuona namna bora ya usimamizi wa miradi ya Jamii. Miradi inayotumia mtandao wa DAWASA na isiyo na utendaji mzuri, uendeshaji wake kuanza kuhamishiwa DAWASCO. Hadi sasa miadi 20 ya Jamii shughuli zake za uendeshaji zimekabidhiwa DAWASCO
|
11
|
Uchimbaji holela wa visima usiozingatia taratibu
|
Kuanzisha utaratibu wa kusajili visima na kutoa vibali. Lengo likiwa ni kupunguza magonjwa yanayosababishwa na maji kutoka kwenye visima visivyo na ubora. Zoezi hili linasimamiwa na Ofisi za Bonde la Wami Ruvu.
|
4.0. Mwisho
Tunatoa wito kwa Wadau na watumiaji wa huduma ya maji Mkoa wa DSM kulipia Ankara za maji kwa wakati, kuepuka wizi wa maji na uharibifu wa miundombinu ya maji, kulinda miundombinu iliyopo nainayojengwa ili huduma ya maji iwe endelevu. Aidha, ulinzi shirikishi wa vyanzo vya maji ni budi upewe kipaumbele katika ngazi zote, pia wananchi kutoa taarifaya ya uvujaji wa maji ili kuweza kupunguza upotevu wa maji.
"MAJI NI UHAI NA USAFI WA MAZINGIRA NI UTU"
JEDWALI NA I
Na
|
Jina la Mradi
|
Mtaa unaohudumiwa
|
Wateja waliounganishiwa majumbani
|
Vituo vilivyojengwa
|
Mfadhili
|
Idadi ya Watu wanaohudumiwa
|
Hali halisi ya mradi
|
|
|
Manispaa ya Ilala |
|
||||
1
|
Jumuia ya Watumia maji Kipunguni
|
Kipunguni B na Mji Mpya
|
37 |
12 |
WSDP
|
7,422 |
100% |
2
|
Kivule/Shule ya Msingi
|
Kivule na Viwege
|
23 |
15 |
WSDP
|
6,138 |
100% |
3
|
Pugu Bangulo
|
Bangulo
|
56 |
6 |
OWN SOURCE
|
6000 |
100% |
4
|
Jumuia ya Watumia maji GOPU
|
Gongolamboto,Ulongoni B, Pugu Bombani, Dunda B, Bane na Guluka kwa lala
|
611 |
52 |
WSDP,BTC
|
29,666 |
100% |
5
|
Ulongoni A
|
Ulongoni A
|
53 |
4 |
Mfuko wa Jimbo
|
2,318 |
100% |
6
|
Jumuia ya Watumia maji Kitunda Relini
|
Kitunda Relini
|
218 |
11 |
African Relief of Kuwait
|
6,808 |
100% |
7
|
Jumuia ya Watumia maji Kitunda C
|
Kiyombo
|
113 |
5 |
DAWASA
|
3,520 |
100% |
8
|
Kitonga
|
Kitonga
|
22 |
3 |
Own Source
|
1,632 |
100% |
9
|
Mkera
|
Mkera
|
- |
3 |
Own Source
|
1500 |
90% |
10
|
Lubakaya
|
Lubakaya
|
- |
4 |
Own Source
|
2,000 |
100% |
11
|
Lukooni
|
Lukooni
|
3 |
3 |
Own Source
|
1,518 |
100% |
12
|
Usambazaji wa maji Pugu Kichangani
|
Kichangani
|
|
16 |
Own Source
|
8000 |
98% |
13
|
Usambazaji maji Kinyamwezi
|
Kinyamwezi,
Mustafa na Viwege |
- |
6 |
Halmashauri ya Jiji
|
3,000 |
100% |
14
|
Jumuia ya Watumia maji Rada
|
Rada
|
16 |
3 |
Maendeleo ya Kata
|
1,596 |
100% |
15
|
Mradi wa maji Pugu Station
|
Pugu Station
|
25 |
6 |
JICA, Own Source
|
3,150 |
100% |
16
|
Mradi wa maji Segerea
|
Segerea
|
- |
4 |
Own Source
|
2,000 |
100% |
17
|
Mradi wa maji Kivule
|
Kerezange na Kivule
|
167 |
9 |
JICA
|
5,502 |
100% |
18
|
Jumuia ya Watumia maji Twiga
|
Tabata Kisiwani na Kimanga darajani
|
50 |
13 |
BTC
|
6,800 |
100% |
19
|
Jumuia ya Watumia maji Ugombolwa
|
Ugombolwa
|
104 |
5 |
BTC
|
3,020 |
100% |
20
|
Kisukuru
|
Kisukuru
|
- |
- |
Own Source, DAWASCO
|
2,500 |
85% |
21
|
Jumuia ya Watumia maji Mzinga A
|
Mzinga
|
620 |
11 |
DAWASA/
WUA MZINGA |
9,220 |
100% |
22
|
Jumuia ya Watumia maji Mzinga B
|
Mzinga
|
270 |
2 |
DAWASA/
WUA MZINGA B |
2,620 |
100% |
23
|
Mradi wa maji Madenge
|
Madenge
|
56 |
4 |
Own Source
|
2,336 |
100% |
24
|
Mradi wa maji Belege
|
Maruzuku
|
34 |
3 |
Own Source
|
1,704 |
Low yield |
25
|
Mradi wa maji Mfenesini
|
Mnyamani
|
52 |
10 |
Own Source
|
5,312 |
100% |
26
|
Mradi wa maji Buguruni moto
|
Kisiwani
|
12 |
3 |
DAWASA
|
1,572 |
100% |
27
|
Jumuia ya Watumia maji Sharif Shamba
|
Sharif Shamba
|
10 |
9 |
Own Source
|
4,560 |
100% |
28
|
Jumuia ya Watumia maji Mondo
|
Mivinjeni
|
26 |
3 |
Own Source
|
1,656 |
100% |
29
|
Kinyerezi
|
|
|
9 |
BTC,DAWASCO
|
4500 |
100% |
30
|
Mradi wa maji Tabata
|
Mtambani
|
- |
3 |
Own Source
|
1,500 |
90% |
31
|
Mradi wa maji Kitunda
|
Kipera
|
- |
7 |
Own Source
|
3,500 |
85% |
32
|
Mradi wa maji Virobo
|
Virobo
|
- |
1 |
Own Source
|
500 |
85% |
33
|
Mradi wa maji Tungini
|
Tungini
|
- |
3 |
Own Source
|
1,500 |
50% |
34
|
Mradi wa maji Majohe
|
Majohe
|
- |
18 |
Own Source
|
9,000 |
35% |
36
|
Mongolandege
|
|
|
5 |
DAWASA
|
2400 |
100% |
37
|
Kipunguni B
|
|
|
5 |
DAWASA
|
2400 |
100% |
38
|
FFU Ukonga
|
|
|
4 |
DAWASA
|
5700 |
100% |
39
|
Kipunguni kwa Mkwelemba
|
|
|
5 |
DAWASA
|
3100 |
100% |
40
|
Kivule Nyang’andu
|
|
|
4 |
DAWASA
|
3100 |
100% |
41
|
Tabata Kisiwani
|
|
|
13 |
BTC
|
6500 |
100% |
|
|
Manispaa ya Kigamboni |
|
||||
1
|
Minondo- Somangila
|
Minondo
|
|
10 |
FOOD Aid Counterpart
|
200 |
75% |
2
|
Mwasonga Kisarawe II
|
Mwasonga
|
|
15 |
FOOD Aid Counterpart
|
200 |
90% |
3
|
Ferry
|
Ferry
|
483 |
12 |
DAWASA, Water Aid
|
22,035 |
100% |
4
|
Kibugumo
|
Kibugumo
|
99 |
9 |
JICA
|
4500 |
100% |
5
|
Mjimwema/ Salanga
|
Salanga
|
71 |
9 |
JICA
|
950 |
100% |
6
|
Tungi
|
Tungi/ Muungano.
|
225 |
9 |
Water Aid
|
5500 |
100% |
7
|
Toamoyo
|
Toamoyo
|
272 |
4 |
Water Aid
|
5132 |
100% |
8
|
Kigamboni
|
Kigamboni
|
266 |
8 |
Water Aid
|
5416 |
100% |
9
|
Chambewa
|
Chambewa
|
0 |
0 |
WSDP
|
938 |
35% |
10
|
Malimbika
|
Malimbika/ Dege
|
0 |
0 |
WSDP
|
3047 |
20% |
11
|
Kibene
|
Kibene/ Majengo
|
0 |
12 |
WSDP
|
5132 |
20% |
12
|
Yale yale Puna
|
Punacenter/Moris/ Kibungo
|
28 |
25 |
JICA
|
2460 |
100% |
13
|
Tundwisongani
|
Tundwi/ Songan/ Nyange
|
7 |
25 |
JICA
|
3721 |
100% |
|
|
Manispaa ya Kinondoni |
|
||||
1
|
Makongo Mbuyuni
|
Makongo Mbuyuni
|
10 |
14 |
WSDP
|
3600 |
100% |
2
|
Makongo Juu
|
Makongo Juu
|
0 |
2 |
World Bank/LGCDG
|
3500 |
100% |
3
|
Tandale
|
Mtogole
Pakacha Mkunduge Mhulitani Sokoni Kwa Tumbo |
80 |
21 |
BTC
|
5347 |
100% |
4
|
Shule ya Msingi Changanyikeni
|
Changanyikeni
|
0 |
2 |
LGCDG
|
1900 |
100% |
5
|
Mabwepande
|
Bunju B, Mji Mpya na Mabwepande
|
500 |
43 |
WSDP
|
11278 |
100% |
6
|
Kigogo Buyuni
|
Kigogo Buyuni
|
0 |
1 |
Own Source
|
1617 |
100% |
7
|
Kigogo Kati
|
Kigogo Kati
|
0 |
2 |
Own Source
|
2100 |
100% |
8
|
Mivumoni
|
Mivumoni
|
0 |
1 |
Own Source
|
589 |
85% |
9
|
Mtambani
|
Mtambani
|
18 |
1 |
Own Source
|
500 |
100% |
10
|
Mwinyimkuu
|
Mwinyimkuu
|
26 |
3 |
Own Source
|
1250 |
100% |
11
|
Magomeni Idrissa
|
Magomeni Idrissa
|
0 |
1 |
Own Source
|
305 |
100% |
|
|
Manispaa ya Temeke |
|
||||
1
|
Toangoma
|
Goroka
|
154 |
14 |
WSDP
|
8,386 |
100% |
2
|
Mbagala
|
Kizinga Bughidad
|
128 |
34 |
WSDP
|
17,152 |
100% |
3
|
Chalambe
|
Mashine ya Maji
|
4 |
7 |
BRN
|
3,528 |
100% |
4
|
Mianzini
|
Mianzini
|
133 |
27 |
WSDP
|
7,947 |
100% |
5
|
Kibondemaji
|
|
|
3 |
Water Aid,PDF, DAWASCO
|
19500 |
100% |
6
|
Mivinjeni
|
|
|
5 |
Own source
|
3000 |
100% |
7
|
Makuka
|
|
|
18 |
Own source,TASAF
|
|
100% |
8
|
Kiembe Samaki
|
|
33 |
8 |
TASAF
|
4,297 |
100% |
9
|
Tandika/ Mabatini
|
Mabatini
|
|
8 |
WSDP
|
11000 |
95% |
10
|
Sandali/ Mamboleo B
|
Mamboleo B na Kisiwani
|
|
8 |
WSDP
|
8000 |
95% |
11
|
Azimio/Mbuyuni
|
Azimio
|
|
7 |
WSDP
|
11500 |
95% |
12
|
Mamboleo A
|
Mamboleo A, Tindwa, Usalama
|
148 |
15 |
Water AID
|
8,332 |
100% |
13
|
Dovya
|
Dovya, Msakala,Uwazi na Mbonde
|
402 |
12 |
BTC
|
11,379 |
100% |
14
|
Mgembaki
|
Mbagala kuu, Kichemchem, Jeshi la wokovu, Mgeni nani
|
658 |
16 |
BTC
|
13,922 |
100% |
15
|
Kiwika- Kijichi
|
Butiama, Misheni,na kijichi
|
464 |
31 |
BTC
|
17,426 |
100% |
16
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa