• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Waziri wa Ujenzi Mhe Bashungwa, RC Chalamila wakagua Ujenzi wa Barabara Chanika- Msongola - Mbande

Posted on: November 15th, 2023

 

Waziri wa ujenzi Mhe Innocent Bashungwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila leo Novemba 14, 2023 wameendelea na ziara na kukagua miradi ya barabara Chanika-Msongola mpaka Mbande

Wakiwasili eneo la Msumbiji, Chanika walikuta jinsi wafanyabiashara walivyopanga bidhaa zao karibu na barabara huku wengine walivyojenga kwenye hifadhi za barabara na kusababisha magari kupita kwa shida hali inayopelekea kuwe na foleni.

Mhe. Bashungwa aliwataka wananchi wa eneo hilo kujiandaa kisaikolojia kuhama katika eneo hilo kupisha ujenzi wa barabara na 'round about' ya kisasa kwasababu wapo ndani ya hifadhi ya barabara na hakuna sheria inayomruhusu yoyote ndani ya mita 22.5 kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1932 hata kama wamepeleka zuio hilo mahakamani.  

Akiwa eneo la Msongola Mhe Waziri alikagua  barabara ya Msongola-Mbande na kujionea jinsi mkandarasi aliyekabidhiwa ujenzi huo akifanya uzembe kwa kisingizio cha mvua na kuchelewesha mradi huo na kupewa mwezi mmoja barabara hiyo iwe imekamilika yenye urefu wa KM 3.8.

Vilevile Mhe. Bashungwa aliwasihi wakandarasi wazawa watumie fursa wanazozipata ili wajitengenezee sifa nzuri, "Ninatoa wito kwa wakandarasi wazawa msitie aibu kama hii tuliyoiona hapa. Wananchi wanapokuona umechukua muda mrefu wanaona ni mbabaishaji."

Mhe Chalamila naye aliongezea, "Nikiri kwanza mkandarasi huyu ana bahati sana nilikuwa sijafika kabla yako Mhe Waziri. Sababu za mvua zipo, vilevile na wengine wameshamaliza miradi hii na mvua ipo, huyu bwana alipaswa kuchukuliwa hatua, na hatua kubwa yakuchukuliwa ni kulala ndani kwanza."

Pia RC Chalamila aliongea na wananchi hao kutokana na changamoto wanazopitia wataandaa mkutano na mkuu wa wilaya  Jumatatu ijayo kuanzia saa 6 mchana mpaka saa 12 jioni kuweza kusikiliza kero wanazopitia zikiwemo athari za mvua zinazoendelea, migogoro ya ardhi na viongozi wala rushwa.

Akitoa salamu kutoka kwa Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan Mkuu wa Mkoa aliwambia wananchi kuwa kutakuwa na awamu nyingine ya kujenga barabara za mwendo kasi ili kuondoa adha ya usafiri sababu upande ule una wananchi wengi, na kuwapa pole wote waliokumbwa na mafuriko

Wananchi nao walioeleza kero wanazozipa zikiwemo  kukosa mifereji, vituo vya daladala, matuta na alama za barabarani, na kulaumu mkandarasi kushughulika na barabara akiona viongozi, huku wengine wakiomba barabara zinazopita ndani ya mitaa zifukiwe kutokana na kuharibiwa na mvua za El-Nino zinazoendelea kunyesha

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa