• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Waziri Mkuu Atembelea Miundombinu iliyohabiriwa na Vurugu za Oktoba 29 Dar.

Posted on: November 24th, 2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya kutembelea miundombinu mbalimbali jijini Dar es salaam ikiwemo iliyoathiriwa na vitendo vya uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 29 na kuelekeza usafuri wa mwendokasi kurejea ndani ya siku kumi huku pia akiagiza kanisa la ufufuo na uzima kufunguliwa ili kutoa haki kwa waumini kuendelea na ibada

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika Mbezi mwisho wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Dkt Mwigulu pamoja na kutoa pole kwa wananchi  amesema usafiri huo wa mwendokasi ambao miundombinu yake imeharibiwa ni muhimu kwa wananchi hivyo ni lazima kufanyike maboresho ya haraka na urejee mara moja huku  akielekeza wizara ya TAMISEMI kuwaamini wakandarasi wazawa kwenye ujenzi wa miradi ya barabara na maeneo mengine ili vijana wa kitanzania wapate ajira.

Aidha ameagiza watumishi wote wazembe na wala rushwa wasihamishwe vituo vya kazi bali wafukuzwe kazi kwani wapo vijana wengi wanaohitaji kupata ajira ambapo amewataka vijana kulinda nchi yao badala ya kushiriki katika vitendo vya uharibifu wa nchi yao huku akiwataka kuiamini tume iliyoundwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia.

Akizungumzia suala la kanisa la ufufuo na uzima kufunguliwa Dkt Mwigulu amesema ni muhimu lifunguliwe na lipewe muda wa miezi sita ya matazamio kwani akifanya kosa kiongozi wa kanisa au msikiti si vyema kuwaadhibu waumini ambapo pia amezungumzia maelekezo ya Rais Dkt Samia kuwa sherehe za maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika 9 Disemba mwaka huu hazitakuwepo na fedha za maadhimisho hayo zitumike kuboresha miundombinu iliyoharibiwa siku ya uchaguzi mkuu.

Awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Waziri wa TAMISEMI Riziki Shemdoe amesema kuwa katika barabara ya kutokea katikati ya Jiji kuja kimara zaidi ya vituo 20 vya mwendokasi vimeharibika pamoja na mifumo muhimu ya ukataji tiketi jambo ambalo limesababisha usafiri huo kusitishwa kwa muda

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amezungumzia baadhi ya athari zilizotokea wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 29 na kuahidi kuendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa amani na kulinda nchi yao pia amesisitiza kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki bila kutoa rushwa ikiwemo vijana kupata mikopo na huduma zingime zikiwemo maji na afya kwani mambo hayo huchangia hasira na chuki za wananchi kwa serikali yao

Naye Waziri wa Mawasiliano na Tekinolojia ya habari ambaye pia ni Mbumge wa jimbo la Kibamba Anjela Kairuki na Waziri wa Uwekezaji Profesa Kilila Mkumbo pamoja na kuwashukiru wananchi na kutoa pole kutokana na vurugu zilozojitokeza siku ya uchaguzi wamewataka vijana kuwa wazalendo kwa Taifa na kuepuka kutumika na watu wasiokua na nia njema kwa Taifa huku wakipongeza kazi ya kuboresha huduma za jamii inayofanywa na serikali huku pia wakiomba stendi ya Magufuli itumike ipasavyo

Matangazo

  • MWENENDO WA BEI WIKI YA 17-21 NOVEMBA 2025 MKOA WA DAR ES SALAAM. November 24, 2025
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Mkuu Atembelea Miundombinu iliyohabiriwa na Vurugu za Oktoba 29 Dar.

    November 24, 2025
  • Katibu Tawala DSM Akutana na Wadau toka CRDB.

    November 26, 2025
  • RC Chalamila Akutana na Wadau wa Nishati ya Mafuta Dar

    November 07, 2025
  • RC Chalamila Atangaza Kurejea kwa Huduma Mbalimbali Dar

    November 05, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa