• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Waziri Lukuvi Ashuhudia Mafanikio Lukuki Ubungo

Posted on: September 18th, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera,Bunge na Uratibu )Mhe. William Lukuvi Leo Septemba 18,2024 ameanza rasmi ziara Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya Ubungo ambapo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Wilaya hiyo ikiwemo miradi ya Maji na Afya.

Mhe. Lukuvi akiwa kwenye ziara hiyo amekagua mradi wa ujenzi wa tenki kubwa la maji eneo la Mshikamano Mbezi, mradi ambao umetekelezwa kwa zaidi ya Bilioni 4 ambao unahudumia zaidi ya watu Laki mbili katika Wilaya hiyo, hivyo kuondoa kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji vilevile amekagua kituo Cha Afya Kimara Saranga ambapo amependezwa na utekelezaji wa mradi huo. "Shukurani nyingi kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, huduma katika sekta ya Afya Wilaya ya Ubungo inapatikana kwa asilimia 100." Alisisitiza Lukuvi.

Aidha Mhe. Waziri Lukuvi akiwa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi Viwanja vya Barafu Kata ya Mburahati-Ubungo amepata wasaa wa kuwasikiliza viongozi mbalimbali katika mkutano huo na kushuhudia yale aliyokagua na kusema kuwa mabadiliko haya ni makubwa sana ikijumuishwa na miundombinu ya barabara itakayomalizika kujengwa ndani ya muda mfupi.

Sambamba na hilo Mhe. Waziri Lukuvi ameahidi kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam kuendelea kuwaonesha watanzania miradi yote iliyotekelezwa chini ya Serikali ya awamu ya Sita pamoja na kutoa fursa kwa wananchi waeleze na kutoa maoni ni kwa namna gani wamekuwa wakinufaika na miradi hiyo mfano Maji, Hospitali, Elimu na mengineyo.

Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Toba Nguvila amemuhakikishia Waziri Lukuvi kuwa hali ya Usalama ya Mkoa ni shwari, una amani kubwa na hali ya utulivu, vilevile wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam wanafanya kazi hasa za biashara ikiwa ni zaidi ya asilimia 90 ni wafanyabiashara  pia utekelezaji wa miundombinu katika sekta mbalimbali ni jambo endelevu na lenye kuleta mafanikio makubwa.

Mwisho ifahamike kuwa ziara ya kuelezea mafanikio ya Mheshimiwa Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan ni endelevu, imeanza Wilaya ya Ubungo na itaendelea Wilaya zingine zote za Mkoa wa Dar es salaam

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa